Burudani ya Michezo Live

Mamba aliyenusurika kufa Vita Kuu ya pili, afariki Dunia

Mamba aliyenusurika kufa Vita Kuu ya Pili mjini Berlin na ambaye kulikua na tetesi- zisizo za kweli- kwamba alikua ni wa kiongozi wa Nazl Adolf Hitler amekufa katika hifadhi ya wanyama iliyoko mjini Moscow.

“Jana asubuhi, mamba huyo aliyefahamika kama Mississippi Saturn alikufa kutokana na uzee. Alikuwa na umri wa miaka takriban 84 – umri wa kuheshimiwa sana ,” ilisema hifadhi ya wanyama.

Saturn alitolewa kama zawadi kwa hifadhi ya wanyama ya Berlin mwaka 1936 muda mfupi baada ya kuzaliwa nchini Marekani. Alitoroka hifadhi ya wanyama baada ya kupigwa mabomu mwaka 1943.

Wanajeshi wa Uingereza walimpata miaka mitatu baadae na kumtoa kwa Muungano wa Usovieti.

Jinsi alivyoishi miaka yote hiyo limesalia kuwa ni jambo la muujiza, lakini tangu Julai, 1946 mamba huyo amekuwa akitembelewa sana na wageni mjini Moscow.

“Hifadhi ya wanyama ya Moscow imekuwa na heshima kubwa ya kumtunza Saturn kwa miaka 74 ,” imesema katika taarifa yake.

“Kwetu sisi Saturn alikua ni enzi nzima, na hilo sio la kutia chumvi hata kidogo… Alituona wengi wetu tulipokua watoto. Tunatumai kuwa hatukumkatisha tamaa .”Embedded video

Hifadhi hiyo ya wanyama iliripoti kuwa mamba Saturn aliwafahamu wanaomtunza, alipenda kubembelezwa kwa kusingwa na brashi-na aliweza kutafuna koleo na sementi kidogo kwa meno yake wakati alipohisi kukasirika.

Mamba huyo wa Mississippi kwa kawaida huishi kati ya miaka 30 na 50 na msituni, iliongeza kusema taarifa kuhusu kifo chake.

Saturn huenda akawa ndiye mamba aliyekuwa na umri mkubwa zaidi duniani- haiwezekani kusema hilo. Mamba mwingine dume, aliyefahamika kama Muja ambaye yuko katika hifadhi ya wanyama ya Belgrade nchini Serbia, pia ana umri wa miaka 80 na zaidi na bado anaishi.

Lakini bila shaka hakuna mamba mwingine anayeweza kushindana na Saturn inapokuja katika suala la kuuza kumbukumbu za matukio yao.

Taarifa yake iliyogonga vichwa vya habari na kuvutia wengi ilikua ni kuhusu maelezo ya tetesi za uvumi kwamba alikuwa ni mmoja wa wanyama binafsi wa Hitler , jambo ambalo lilikua si sahihi.

“Muda mfupi baada ya kuwasili kwa mnyama huyo, uvumi ulijitokeza kwamba alikuwa ni mmoja wa wanyama wa Hitler, na sio kutoka katika hifadhi ya wanyama ya Berlin,” Shirika la habari la Interfax liliripoti.

Haijawa wazi ni vipi tetesi hizo zilianza.

Hifadhi ya wanyama ya Moscow ilipuuzilia mbali ripoti za aina hiyo, ikasema wanyama ”sio wanasiasa na hapaswi kuwajibishwa na madhambi ya binadamu “.

Mamba anayehangaisha wakaazi

Jinsi Suturn alivyoweza kunusurika kifo alipotoroka mwaka 1943 huenda likawa jambo lisiloweza kupatiwa jibu kamwe.

Berlin, ambao ulikua ni mji mkuu wa Nazi Ujerumani, ulipigwa mabomu mengi kabla ya kumalizika kwa vita mwaka 1945.

Kile kilichoitwa Mapigano ya Berlin yalianza 1943 na usiku wa 22-23 Novemba ulishuhudia mapambano yaliyosababisha uharibifu mkubwa wa maeneo ya magharibi ya kati, ikiwa ni pamoja na wilaya ya Tiergarten ambako ndiko iliko hoifadhi ya wanyama alimokuwemo mamba Saturn.

Melefu ya watu Twaliuawa au kujeruhiwa na wanyama waliokuwa katika hifadhi ya wanyama waluliwa pia.

Jengo la hifadhi ya wanyama lililengwa kwa mambomu moja kwa moja. Ripoti moja ilisema kuwa maiti za mamba wane zilionekana nje zikigaagaa kutrokana na nguvu ya mlipuko.

Saturn alinusurika kwa bahati na akaishi kwa miaka mitatu katika jiji lililosambaratishwa na vita, na hali ya hewa isiyoyofaa kwa mamba.

Imeripotiwa kuwa sasa atakaushwa na kuwekwa katika jumba la makumbusho ya kibaiolojia lilililopewa jina la Charles Darwin.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW