Shinda na SIM Account

Mambo 10 usiyoyafahamu kuhusu mchezaji mpya wa Barcelona Yerry Mina

Barcelona ilifanikiwa kumsajili mchezaji, Yerry Mina kutokea katika timu ya Palmeiras siku ya Alhamisi ya wiki hii kwa mujibu wa klabu hiyo ya Hispania.

Mina mwenye umri wa miaka 23, raia wa Colombia ametua  Camp Nou kwa dau la euro milioni 11.8.

Na haya ndiyo mambo 10 usiyoyafahamu kuhusu Yerry Mina

1.Raia wakwanza wa Colombia kuichezea Barcelona

Yerry Mina atakuwa Mcolombia wakwanza kucheza rasmi na FC Barcelona. Lauro Mosquera alicheza mchezo wa kirafiki pekee dhidi ya  Sabadell  Juni 24, mwaka 1964 lakini hakuwa rasmi ndani ya timu hiyo.

2.Yupo katika kizazi sawa kama Denis Suárez

Anashirikiana siku ya kuzaliwa na (1994) na Denis Suárez. Kiungo huyu wa Blaugrana amezaliwa January 6, Mina hadi Septemba atakuwa anatimiza miaka 23.

3. Mchezo wake wa kwanza na timu yake ya Colombia

Mina amecheza mchezo wake wa kwanza na timu yake ya taifa Oktoba 6, mwaka  2016, na bao lake la kwanza akifunga Oktoba 11 ambao ulimalizika kwa sare ya 2-2 dhidi ya Uruguay.

4.Mchezaji mrefu zaidi Barça

Beki huyo wakati amekuwa ni mchezaji mrefu zaidi wa  1.95m, ndani ya Barcelona na kuwazidi wenzake  Piqué (1.94m), Sergio (1.89m) and Andre Gomes (1.88m).

5.Ni mchezaji wa 10 wa Colombian ndani ya ligi ya La Liga

Yerry Mina anakuwa mchezaji wa 10 kutoka Colombian kucheza ligi ya Hispania  akijumuika na wenzake kama Carlos Bacca (Villarreal), Juanjo Narváez (Real Betis), Luis Muriel (Seville), Daniel Torres (Alavés), Jefferson Lerma (Levante), Jeison Murillo (Valencia) na Bernardo Espinosa, Johan Mojica na Marlos Moreno (Girona).

6.Anacheza zaidi ya namba nne

Yerry Mina amekuwa na uwezo wa kucheza namba nne hapo awali. Namba 3 akiwa Deportivo Pasto, namba 26 akiwa  Independiente Santa Fe and Palmeiras, namba 13 na 16 akiwa na timu yake ya taifa ya Colombian.

7. Ana taasisi inayojulikana kama Yerry Mina Foundation

Mchezaji huyu ana taasisi yake iliyoanza mwishoni mwa mwaka 2016 huko Guachené, umbali wa kilomita 30 kutokea Cali,ukiwa na lengo la kuwasaidia wa 2,000.

 8. Akitokea kuwa mlinda lango mpaka mlinzi wa kati
Mina ameanza mchezo wa soka akiwa kama golikipa,katika michezo ya asili akiwa na familia yake lakini baadae ndipo akaamua kubadili nafasi.
9. Mataji aliyochukua
Mcolombia anaendelea kuwa mchezaji muhimu huku akichukua mataji kadhaa. Mina amechukua ubingwa Colombia mwaka 2014, akishinda Copa Sudamericana mwaka 2015 na Brasileirao akiwa Palmeiras mwaka 2016.
10. Familia na marafiki
Familia ya Mina na marafiki zake ni muhimu katika maisha yake na hutumia muda mwingi nje ya Uwanja akiwa nao  kama wanavyoonekana katika picha ambayo aliweka katika mitandao yake ya kijamii.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW