Tupo Nawe

Mambo 7 usiyoyajua kuhusu uongozi wa Omar al-Bashir Sudan, kabla ya kupinduliwa na Jeshi la nchi yake

Mapinduzi ya Alhamisi nchini Sudan huenda yaliweza kumg’oa madarakani rais ambaye hakupendwalakini kwa wale waliokuwa karibu na Omar al-Bashir wameazimia kubakia madarakani are , ameandika mtaalamu wa Sudan Alex de Waal. Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka karibu 30, Sudan haitawaliwi na Rais Omar al-Bashir.

Lakini wakati Wasudan walipomsikiliza Luteni Jenerali Awad Ibn Ouf akitangaza baraza la mpito la kijeshi, walihisi ni kama wanasikia sauti ya mkuu wake.

Kwa mujibi wa BBC. Gen Ibn Auf ni mwanajeshi mwenye taaluma ya jeshi, mshirika wa karibu wa Bwana Bashir. Akikuwa mkuu wa ujasusi wa jeshi wakati wa mzozo na maafa katika jimbo la Darfur, ambapo alikuwa kwenye orodha ya Marekani ya watu wanaolengwa kwa vikwazo vya kifedha.

Waandamanaji mjini Khartoum
Image captionHaikutajwa kma raia watahusishwa katika kipindi cha mpito cha miaka miwili

Alikuwa waziri wa ulinzi na baada ya rais Bashir kutangaza hali ya tahadhari tarehe 22 Februari , Generali Ibn Auf pia alipandishwa cheo na kuhudumu kama makamu wa rais, ishara kuwa atamrithi rais Bashir wakati muhula wake utakapomalizika Aprili 2020.

Kilichochochea kuondolewa kwa Bwana Bashie mamlakani yalikuwa ni muendelezo wa maandamano ya amani ya mfululizo ya siku tano ambapo maelfu kwa maelfu ya watu waliozingira makao makuu ya jeshi mjini Khartoum walimtaka rais aondoke madarakani.

Mgawanyiko wa viongozi

Lakini kile kilichotokea kilitokana na mazungumzo magumu baina viongozi waliokuwemo ndani ya majengo hayo ya jeshi, miongoni mwa wakuu wa kijeshi ambao walikuwa chini ya rais katika vyeo vyao vya kijeshi.

Wakati tukio hilo lilipotangazwa Alhamisi , kulikuwa na ukimya usio wa muda mrefu kwenye makao makuu ya jeshi wakati Jenerali Ibn Auf, makamanda wa jeshi la Sudan na maafisa wengine muhimu wa ngazi ya juu jeshini kama vile Jenerali Salah Abdalla Gosh, Mkuu wa Shirika la Taifa la Ujasusina huduma za usalama (NISS), wakilumbana juu ya kipindi cha mpitpo cha kisiasa kitakachofuatia baada ya kuondolewa madarakani kwa Bwana Bashir.

Omar al-Bashir ni nani:

Rais Omar al-Bashir
  • Alipigana katika jeshi la Misri mnamo mwaka 1973 katika vita kari ya Waarabu na Israeli
  • Alinyakuwa mamlaka nchini Sudan mwaka 1989 katika mapinduzi yaliyoungwa mkono na waislamu
  • Ni mkuu wa nchi wa kwanza aliyeshtakiwa na mahakama ya ICC mwaka 2009, lakini anakana shutuma za uhalifu wa kivita jimboni Darfur
  • Alifikia makubaliano ya amani na waasi wa sudan Kusini mwaka 2005
  • Alishuhudia kushuka kwa uchumi wa Sudan Kusini 2011, na kusababisha Sudan kupoteza theluthi tatu ya utajiri wake wa mafuta
  • Alipinduliwa mwezi Aprili 2019
  • Maisha yake binafsi hayajulikani sana. Hana mtoto
Wengine walisherehekea Khartoum baada ya tangazo hilo

Wakati Gen Ibn Auf alipohutubia taifa , alitangaza kuondolewa kwa Rais Bashir, kuvunjwa kwa katiba , kuundwa kwa baraza la mpito la jeshi, hali ya tahadhari na kipindi cha mpito cha miaka miwili . lakini hakuwakaribisha wawakilishi wa upinzanikatika serilkali. Hakutaka hata kutoa fursa ya mazungumzo na upinzani.

maelezo ya mkataba miongoni mwa wakuu wa usalama hawajatangazwa kwa umma. Lakini matokeo yake ni wazi.

Kuepuka umwagaji damu mitaani.

Kwanza, jeshi , NISS na viongozi wa bunge (kama vile Mohamed Hamdan “Hemeti”, (kamanda wa kikosi cha dharura) wanataka kuwe na mgawanyo wa mamlaka miongoni mwao.

Wanataka kuepuka kurudia makabiliano kama yaliyotokea mapema wiki hii, wakati wanajeshi walipowafyatulia risasi wanamgambo wa NISS waliokuwa wakijaribu kuutawanya umati mkubwa wa waandamanaji kwa kunguvu , ukiachana na vita vya pande mbili kwenye mitaa ya mji mkuu.

Pili , wakuu wa jeshi wanaushirika na Misri, Saudi Arabia na Milki za kiarabu. Wakati huo huo, Qatar na Uturuki wamepoteza.

Uongozi mpya ulivunja chama tawala cha National Congress Party (NCP) na wameripotiwa kuwakamata wengi miongoni mwa makaka wakongwe wa kiislamu (Muslim brotherhood).

Rais Omar al-Bashir (katikati) alipoingia madarakani kwa mapinduzi mwaka 1989
Image captionRais Omar al-Bashir (katikati) alipoingia madarakani kwa mapinduzi mwaka 1989

Wanang’ang’ana kufiarifu nchi za magharibi kwamba Waislamu walipanga mapinduzi , ambayo yalihitaji kufuatiwa na jeshi kuchukua mamlaka ,na kwamba waandamanaji wanaodai demokrasia pia ni makaka wa kiislamu

Jenerali Ibn Auf na washirika wake si dhaifu kiasi cha kufiria kwamba watauridhisha upinzani kwa kauli hiyo. Ila wanachokifanya ni kuvuta muda ili waweze kuamua ikiwa watafuata njia ya ukandamizaji au njia nyingine mbali mbali.

Sudan imepiga hatua moja nyuma kutoka kwa umwagaji damu kwenye mitaa ya mji mkuu, lakini ni moja tu. Ikiwa mapinduzi ya 11 Aprili yatakuwa ni hatua ya kuelekea demokrasia , itakuwa ni kinyume na walichokitaka waliofanya mapinduzi, sio kwasababu yao.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW