Habari

Mambo 9 aliyoyasema Makamu wa Rais Dodoma leo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu leo amezungumza mambo mengi katika uzinduzi wa programu ya kuifanya Dodoma iwe ya kijani.

Haya ni baadhi ya mambo 9 aliyoyazungumza mjini Dodoma;

-Tupunguze ukataji miti na uvunaji wa miti uzingatie sheria zilizopo.

-Taasisi za serikali zitunge sheria ndogo za kusimamia shughuli za mazingira.

-Wananchi tuitikie na kutekeleza programu mbalimbali zinazoanzishwa kwa ajili ya utunzaji wa mazingira.

-Hii ni awamu ya kwanza tutaratibu awamu ya pili ya program hii.

-TANROADS iandae utaratibu wa kupanda miti pembezoni mwa barabara.

-Wananchi tuanze kutumia nishati mbadala ili kunusuru mazingira yetu.

-Naagiza kampeni hii isiishie Dodoma Mjini bali ienee katika Wilaya zote za Mkoa huu na hatimaye nchi nzima.

-Upandaji wa miti si kwa ajili ya hifadhi tu bali ni fursa ya kiuchumi pia.

-Kampeni hii ya kuufanya mji wa Dodoma kuwa kijani ni kuunga mkono uamuzi wa Rais wetu Dkt. Magufuli wa kuhamishia Makao Makuu hapa Dodoma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents