Michezo

Mambo makuu manne usiyoyajua Simba vs Mtibwa wikiendi hii

Wikiendi hii Ligi Kuu Tanzania Bara itaendelea kutimua vumbi katika viwanja mbali mbali wakati uwanja wa Uhuru wa jijini Dar es laam siku ya Jumapili hii kutakuwa na mchezo wa upinzani mkali baina ya Simba ya jijini Dar es laam dhidi ya Mtibwa Sugar FC kutoka mkoani Morogoro utakaopigwa majira ya saa 10:00 jioni.

 

Mchezaji wa timu ya Mtibwa Sugar, Hassan Isihaka (kulia) akimiliki mpira mbele ya Kichuya  (ushoto)

Upinzani wa mchezo huo wa Jumapili baina ya Simba SC dhidi ya Wakata Miwa wa Manungu, Turiani, mkoani Morogoro timu ya Mtibwa unatokana na mambo makuu manne ambayo huu fanya hasa kuwa wa kipekee.

Wachezaji waliotumikia vilabu vyote viwili

Baadhi ya vitu vitakavyo ongeza hali ya ushindani uwanjani ni wachezaji waliotumikia vilabu hivi viwili kwa nyakati tofauti na bado wanavitumikia hadi sasa na wanataraji kuwa sehemu ya mchezo siku ya Jumapili.

Jumla ya wachezaji 13, wametumikia vilabu hivi kwa nyakati tofauti na wanataraji kuwa sehemu ya mchezo Jumapili hii katika uwanja wa Uhuru. Simba ina jumla ya wachezaji 8 waliotokea kwa wana tam tam ambao ni Mzamir Yassin, Shiza Ramadhan Kichuya, Juma Ndanda Luizio, Mohamed Ibrahim”Moudy Cabaye”, Jamal Mnyate, Said Mohamed Nduda, Salim Abdallah Mbonde, Ally Shomary.

Wakati kwa upande wa pili wana tam tam wao wana jumla ya wachezaji watano waliowahi kutumikia klabu ya Simba kwa nyakati tofauti ambao ni Salum Kupela Kanoni, Hassan Isihaka, Henry Joseph, Haruna Chanongo na Issa Rashid “baba Ubaya” ambaye alitokea Mtibwa Sugar kwenda Simba na baadaye akarejea Mtibwa Sugar.

Record za Zuber Katwila “Puchetino” dhidi ya Timu za Dar es laam ambazo ni Simba,Yanga na Azam FC.

Zuber Katwila ni kocha mkuu wa kikosi cha wana tam tam akipokea kijiti kutoka kwa Salum Shaban Mayanga katikati ya msimu wa ligi kuu 2016-2017 ambapo toka aliporithi  nafasi hiyo hakupoteza mchezo wowote wa Ligi Kuu Bara dhidi ya timu za Dar es laam, wikiendi hii anakutana na Simba ambao mchezo wa mwisho kukutana kwao timu hizi zilitoka sare ya bila kufungana kikosi cha wanaramba ramba kikiongozwa kwa mara ya kwanza na Katwila.

Msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu

Mtibwa Sugar imejikusanyia jumla ya pointi sawa na watakao kuwa wenyeji wao siku ya Jumapili Simba, kila timu ikiwa imekuisanya alama 11 na huku ikiongoza msimamo wa ligi kwa tofauti ya magoli ya kufunga.

Kutokana na kila timu kukusanya idadi sawa ya pointi mchezo huo utakuwa na ushindani mkubwa wa kila mmoja kutaka kumshusha mwenzake katika mbio za kuongoza ligi na hali  hiyo itaongeza hamasa ya ushindani katika mchezo huo.

Kutopoteza mchezo wowote

Simba na Mtibwa Sugar zote zita ingia uwanjani zikiwa hazina rekodi ya kutopoteza mchezo wowote wa Ligi Kuu Bara huku kila mmoja akiwa ameshinda michezo 3 na kutoka sare 2, hali hii inaongeza hali ya ushindani katika mchezo huu na kuufanya wa kipekee na kila timu ita ingia uwanjani imejidhjatiti kuibuka na pointi 3 muhimu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents