Habari

Mambo matano yanayosaidia kukuza taaluma yako

Kwanini kukua kwako na kuendelea kunahitajika sana? Ni muhimu katika kuleta changamoto na wewe mwenyewe kujiongeza zaidi na wala usilete maneno ya kuwa umetingwa na kazi zaidi sehemu ambayo huwezi kukua na kujifunza zaidi.

black-business-woman05-750x410

Kuna uwezo kwa kila mtu zaidi ya vile tunavyoona na kujua, hivyo ni muhimu kwa kila mmoja wetu kukua na kuongezeka binafsi na taaluma yake pia. Hii si tu ili upate kazi bora zaidi lakini pia inakufanya ufanye kazi kwa ufanisi na kujitosheleza zaidi. Hapa kuna mambo matano ambayo unaweza kuyafanya binafsi bila msaada ya kampuni au shirika unalofanyia kazi,

1.  Chukua changamoto mpya

Hii inaweza kuwa hatari kwa wakati mwingine na kuchanganya wakati mwingine ingawa inategemea na shirika na kampuni uliyopo. Wakati mwingine changamoto huonekana kujitokeza mara kwa mara wakati hujamaliza ile ya kwanza lakini hiyo inaonyesha unakua na kukamaaa hivyo fursa zikijitokeza utakuwa wa kwanza kuzikumbatia.

  1. Soma.

Unahitaji kusoma sana na si tu masomo ya darasani bali majarida mengi yanayohusiana na taaluma yako na vitabu vyenye tafiti mbalimbali inasaidia kukuongeza ufahamu zaidi wa mambo mengi kwenye taaluma yako na kuwa na wigo mpana katika kushughulikia matatizo.

  1. Wekeza katika kujifunza

Kuna masomo mengi yanatolewa bure kwenye mitandao mbalimbali, tenga muda wako ili uweze kujiongezea ufahamu kwa njia ya mtandao.

  1. Pata mkufunzi wako

Hebu tafuta katika shirika hilo unalofanyia kazi na uone kama kuna mtu ambaye anaweza kuwa mkufunzi wako wa mambo ya taaluma. Kama hakuna tafuta nje ya taasisi hiyo kwa mtu mwenye uelewa zaidi kuliko wewe na mwenye haiba ambayo unaweza kujifunza kutokakana na maisha yake na taaluma yake pia. Ni muhimu kuwa na mawasiliano ya karibu na mtu ambaye unataka kujifunza kwake.

 

  1. Jizingire na watu wenye uelewa na ufahamu kama wa kwako..

Hakikisha marafiki zao na watu wako wa karibu ni wenye uelewa kama wa kwako na mitazamo yako ya kuendelea kukua na kujifunza. Watu wenye akili ambazo hazina moyo wa kujifunza na kukua achana nao, hawatakuelewa sasa lakini baadaye watakuelewa. Kila siku kuna fursa ya kujifunza na kujiboresha katika fikra na utendaji wako kwenye taaluma yako. Hakuna namna nyingine lazima tukue kutoka hapa tulipo na kuweza kufanya mambo makubwa laini inaanzia kwenye fikra binafsi.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents