Aisee DSTV!

Mambo matatu muhimu yatajwa miaka mitano ya M-Pawa

Benki ya CBA ikishirikiana na kampuni ya Vodacom imefanya droo yake ya 5 ya kuadhimisha miaka 5 ya
huduma ya MPawa yenye lengo la kuongeza ushirikishwaji wa kifedha kwa wateja wake kwenye makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam.

Katika kusherehekea maadhimisho hayo, promosheni hiyo inajumuisha droo za kila wiki zilizohusu kuwekeza na kukopa na MPawa huku ukitoa washindi zaidi ya 340 walioibuka na mara mbili ya akiba zao kuanzia kiwango cha Tsh 1000-200,000, simu janja na muda wa maongezi.

Katika kuongelea kuhusu huduma hii ya MPawa, Meneja Masoko wa benki hiyo Bw Solomon Kawiche
aligusia mambo 3 muhimu kwenye maadhimisho hayo ya Miaka 5.

M-Pawa inasherehekea miaka 5, ni mafanikio gani yameonekana tangu kuanzishwa kwa huduma
hii?

Mpawa ilianza na wateja wanne tu ila hadi leo hii imefikisha wateja Mil 8.5 na imefanikiwa kurahisisha Maisha ya wananchi wengi ambao wapo mbali na huduma za kibenki kwa kuwapatia huduma nafuu za kibenki ikiwemo kukopa kiasi kidogo cha hadi 1000 ambacho hauwezi kupata kupitia huduma za benki.

M-Pawa imefanikiwa kutoa huduma ya kuhifadhi akiba kwa kiwango cha chini cha hadi Tsh 1, hakuna benki
nyingine ndani ya Tanzania inayotoa huduma kama hii na kurahisisha huduma za kibenki bila ya kuwa na
utaratibu mrefu kukamilisha miamala.

Watumiaji wa M-Pawa hawana haja ya kutembelea matawi yetu na kupitia huduma hii, wateja wetu wanapata faida kupitia akiba zao. Akiba za wateja wa MPawa pia zipo kwenye usalama wa hali ya juu kwasababu hakuna makato au gharama zilizofichika.

M-Pawa imeinua hali ya Maisha ya mamilioni ya watanzania hususani wafanyabiashara wadogo na bila
kusahau kuwa imekuwa ikitoa uhakika wa kifedha wakati wa dharura; mteja anaweza kukopa muda
wowote na wakati wowote ule.

Nini malengo ya baadae ya M-Pawa?

Ikiwa ni huduma ya kwanza ya kidigitali Tanzania, M-Pawa itaendelea kugusa miasha ya wananchi wengi
ambao wapo mbali na huduma za kibenki na itaendelea kujidhatiti kwenye kuwajumuisha kifedha wateja
wake. Kama benki, tuna maleno ya kuwekeza zaidi kwenye huduma hii kuhakikisha kuwa inaendana na
maendeleo ya sasa ya kisayansi na Teknolojia na kuwezesha huduma hii kwenye application.

Nini maoni yako kwenye huduma za kifedha za kiditali hususani M-Pawa?

Huduma za kifedha za kidigitali kwenye dunia ya leo ni sio kitu ya kupuuza hususani huduma kama
MPawa kwa sababu ya urahisi wake kwenye gharama, uaminifu wake na urahisi wake katika kuitumia.
MPawa inapatika kupitia simu yoyote ya mkononi, ni huduma ya kibenki iliyorahisishwa kutumia mahali
popote kwa gharama nafuu na humpatia mteja faida kupitia akiba anayoweka bila kuwa na gharama
zilizofichwa. Hili linaupa upekee huduma hii ya M-Pawa.

Mshindi mkubwa wa maadhimisho haya ya Miaka 5 ya M-Pawa ataibuka na zawadi ya Million 15 za
kitanzania kwenye droo ya mwisho ya promosheni hiyo.

Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma hii, wateja wanaweza kutembelea mitandao ya kijamii ya benki ya
CBA/Vodacom au kutembelea menyu ya MPawa kwa kubonyeza *150*00# kupitia mtandao wa

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW