Bongo5 Makala

Mambo Mseto: Show ya Radio Citizen/TV yenye mchango mkubwa katika muziki wa Bongo Flava nchini Kenya

mseto

Wakati mwingine jitihada za mtu mmoja zinaweza kuleta mabadiliko makubwa katika jambo ama mambo fulani. Kwa muda mrefu Tanzania na Kenya zimekuwa na ushirikiano mkubwa katika masuala mbalimbali ya kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Kikubwa kinachoziunganisha nchi hizi mbili kiitumaduni ni lugha ya Kiswahili. Kimuziki Kenya na Tanzania zimekuwa karibu pia ambapo radio nyingi za Tanzania zimekuwa zikicheza nyimbo za wasanii wa Kenya na radio Kenya zikifanya hivyo hivyo.

Wanamuziki wa Tanzania hawana budi kuutambua mchango mkubwa wa kipindi cha Mambo Mseto cha Citizen TV ambacho huendeshwa na mtangazaji maarufu nchini humo Mzazi Willy M. Tuva. Ni mtangazaji anayesikilizwa sana nchini Kenya na show yake ya Mambo Mseto jana imetimiza miaka saba tangu ianzishwe.

Tuva akiwa na Diamond
Tuva akiwa na Diamond

Show hiyo hucheza nyimbo za wasanii wa Afrika Mashariki ilianza upande wa radio na mwaka jana kuanzishwa rasmi kwenye televisheni ambapo hucheza video zao.Show hiyo imekuwa na mchango mkubwa mno katika kuutangaza muziki wa Bongo Flava nchini Kenya na hata muziki wa Uganda nchini humo.

Mara kwa mara Tuva amekuwa mstari wa mbele kuzipigia promo nyimbo mpya za wasanii wa Tanzania na wengi wanapaswa kumshukuru kwa moyo wake.Akizingumza jinsi kipindi hicho kilivyoanza, Tuva alisema:

“Nilikuwa nafanyiwa orientation, ilikuwa siku yangu ya kwanza kuingia kazini hapa. Kuna jamaa mmoja alikuwa ana-host show ya mchana lakini hakukuwa na Mambo Mseto. Patrick Kanyeki ndiye alikuwa mchana. Alijua Tuva anakuja hiyo siku kwa hivyo hakukuja. Basi nikaambiwa niingie na hata sikuwa nimejipanga. Niliingia studio nikashika mic na Mambo Mseto ilizaliwa.Hakukuwa na show ya muziki ya East Afrika, basi nikapata idea ya kuifanya.” (Ghafla).

Tuva alipokuwa akipokea tuzo ya Wimbo bora wa Afrika mashariki Kigeugeu kwa niaba ya Jaguar katika tuzo za Kili mwaka jana
Tuva alipokuwa akipokea tuzo ya Wimbo bora wa Afrika mashariki Kigeugeu kwa niaba ya Jaguar katika tuzo za Kili mwaka jana

Tuva anaendesha kipindi maarufu kwa muziki wa Afrika Mashariki ambacho umaarufu wake tunaweza kuufaanisha na XXL ya Clouds FM ama Power Jams ya East Africa Radio. Wimbo wa msanii wa Kenya hauwezi kuhit kama usipopita kwenye show hiyo. Size 8 alisimulia jinsi mtangazaji huyo alivyo na mchango mkubwa kwenye maisha yake ya muziki kwa kusema:

“Nakumbuka tulikuwa studio tumeketi na akina Jua Cali. Hiyo ndiyo ile time nilikuwa nimetoa Size 8, nilikuwa naitwa Linet back then. Akina Jua Cali walikuwa wananiambia kabla ngoma i-hit, lazima ipitie kwa mkono ya Mzazi. Kwa hivyo hiyo ndiyo ilikuwa wish yangu, ngoma yangu ichezwe Mambo Mseto.

Nakumbuka nikienda Citizen radio nimesimama hapo nje, nimenyeshewa, natetemeka nikikungojea. Sijui kama unaweza kumbuka hiyo siku. Halafu ukakuja, ukachukua ngoma yangu, lakini haukuenda. Ni kama uli-notice sikuwa sawa. Ukaniuliza shida ni nini. Nikakuambia mimi hata sina fare. Ukaniuliza mahali naishi, nikakuambi Kariobangi South.

Ulichukua gari yako ukanipeleka mpaka Jogoo Road. Halafu bado haukuniacha hivyo, unakumbuka? Ukanipatia mia mbili na fare kutoka hapo ilikuwa tu 30 bob. Kwa hivyo, mimi Mambo Mseto imenilea kimziki na pia njia ingine. Na-appreciate sana.”(Ghafla).

Kuonesha ukaribu mkubwa na wasanii wa Tanzania, Tuva ameonekana kwenye video ya Kwaajili Yako ya Hussein Machozi na Kesho ya Diamond.Hivi karibuni Tuva alishinda vipengele viwili kwenye tuzo za Nyota (MSETO – BEST TV SHOW & MZAZI – BEST PRESENTER).

Bongo5 inapenda kuitakia birthday njema show hiyo Mambo Mseto na kuishukuru kwa mchango wake katika muziki wa Bongo Flava.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents