Habari

Mambo na vijimambo: Vazi la harusi lililotengenezwa kwa kutumia Condom, na lingine Toilet Paper!! (picha)

Well, ni jambo la kushangaza right? Kusikia gauni la bi harusi limetengenezwa kwa kutumia mipira ya kinga (condoms), na unaweza ukahisi ni utani, ila si utani sababu lipo na ukihitaji moja unaweza kulipata kama utawasiliana na wahusika!! LOL!

PICEDITOR-ILM
Vazi lililotengenezwa kwa kutumia condom

Ijumaa iliyopita mtandao wa Illawarra Mercury wa Australia uliripoti kuwa kituo cha afya cha Illawarra Shoalhaven Local Area Health Service HIV and Related Programs Unit kimetengeneza vazi la bi harusi kwa kutumia condoms.

Vazi hilo limetengenezwa kama njia ya kuongeza ufahamu juu ya ongezeko la maambukizi ya Chlamydia.

Kama haitoshi wiki iliyopita wanamitindo mbalimbali huko Marekani walitengeneza mavazi ya harusi kwa kutumia ‘toilet paper’.

Vazi la harusi lililotengenezwa kwa toilet paper
Vazi lililotengenezwa kwa kutumia toilet paper!

Mavazi hayo yailitumika katika shindano la nguo za harusi zilizotengenezwa kwa kutumia toilet paper, ‘Toilet Paper Wedding Dress Contest’.

Hii inamaanisha ni haya mavazi ni ya kutumia na kuflash sababu huwezi kufua condom wala toilet paper.Funny!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents