Burudani

Mambo ni moto Sauti za Busara Zanzibar

Hatimaye tamasha kubwa la muziki Afrika Mashariki, Sauti za Busara limefunguliwa rasmi leo katika eneo la Ngome Kongwe kisiwani Zanzibar.

Mkurugenzi wa Tamasha la Suati za Busara, Yusuf Mahmoud

Tamasha hilo la 15 litaanzwa kwa kushereheshwa na gwaride la Carnival kuanzia maeneo ya Kisonge Town hadi Michenzani huku likinogeshwa na kundi la Festival Dance Mob linaloongozwa na Haba na Haba kutoka jijini Dar Es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Mratibu wa Tamasha hilo Yusufu Mahamoud amesema kuwa tamasha hilo limeanza rasmi leo na litadumu kwa siku nne mfululizo kwa ajili ya kuleta burudani na vionjo vya muziki kutoka sehemu tofauti duniani.

“Gearide hili ni burudani ya aina yake ambalo linakupa muongozo wa tamasha lilivyo na haupaswi mtu kukosa kwani utakuwa unakosa kuona na kufaidi uhondo wa muziki wa mataifa mbalimbali duniani waliokuja kuonyesha radha na utamaduni wao,” amesema.

Vile vile Yusuf alisisitiza kuwa “Tamasha hili sio tu kutoa burudani bali pia limekuwa likitangaza taifa letu la Tanzania pamoja na vivutio vyake.”

Licha ya chang’amoto zilizopo za wadhamini ila tamasha la Sauti za Busara limekuwa likikusanya watu kutoka mataifa mbalimbali kushuhudia muziki wenye vionjo tofauti.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents