Michezo

Mambo usiyoyafahamu kwenye mechi ya Real Betis na Madrid

Mchezo wa Real Betis na Real Madrid ulikuwa ukitolewa macho zaidi katika La Liga kutokana na uhasimu wa timu hizo mbili zinapokutana.

Hata hivyo Madrid waliibuka na ushindi wa mabao 5-3 kwenye mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Benito VillamarĂ­n. Je unafahamu baadhi ya mambo yaliyotokea kwenye mchezo huo?

Katika mchezo huo Kati za njano nane zilitolewa na mwamuzi wa mchezo huo. Madrid walipata kadi tano za njano na Betis walipata kadi tatu.

Kwa upande wa umiliki mpira, Betis walifanikiwa kutawala kwa kiasi kikubwa mchezo huo kwa asilimia 58 dhidi ya asilimia 42 ya Real Madrid. Wakati huo huo, Betis walifanikiwa kupiga mashuti 20 huku mashuti matano pekee ndio yakilenga goli, nao Madrid walifanikiwa kupiga mashuti 12 na tisa ndio yaliolenga goli la Betis.

Kwenye kona Real Betis walifanikiwa kupata kona 7 na kwa upande wa Madrid walipata kona 5.

Madrid walionekana kuwa na uchu mkubwa wa kutafuta mabao kutokana na kuotea mara tano wakati Batis wakiwa hawakuotea hata mara moja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents