Habari

Mambo yamharibikia Mr. Nice tena, Grandpa Records ya Kenya yamtema

Ni miezi miwili tu imepita toka msanii wa Tanzania ambaye ndie mwanzilishi wa style maarufu ya Takeu, Nice Lucas Mkenda maarufu kama Mr. Nice kupata deal ya kusaini mkataba na studio ya Grandpa Records ya Kenya kwa lengo la kujaribu kumrudisha kwenye ramani ya muziki na kumtangaza zaidi Kenya, lakini..

nice-2

Taarifa mpya na za kushtusha zinasema hatimaye Grandpa imetoa tamko kuwa imesitisha mkataba huo na sasa Mr. Nice sio sehemu ya Grandpa tena kutokana na sababu kadhaa zilizotolewa. Kwa Mujibu wa mtandao wa Ghafla, tamko rasmi la studio hiyo limezitaja sababu za kutoendelea kufanya kazi na msanii huyo mwenye jina kubwa Afrika Mashariki kuwa, ni msanii mgumu sana, asiye na ushirikianao, mvivu, na asiyeaminika ambaye hawajawahi kufanya nae kazi. “the most difficult,uncooperative,lazy,unreliable artist” .

Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa Nice alivunja makubaliano waliyowekeana na label hiyo, na kuwa alikuwa ame sign mkataba na studio nyingine Tanzania kitu ambacho aliwaficha Grandpa mwanzoni wakati wanaingia makubaliano ya kufanya kazi.

Nice wakati wa utambulisho wake kama member mpya wa familia hiyo ya Grandpa alifanya wimbo wa kushirikiana na DNA ambaye yuko chini ya label hiyo, na tayari walikuwa wameanza kuzunguka naye katika tour Kenya nzima kwa lengo la kumtangaza zaidi na kurudisha heshima aliyokuwa nayo hapo awali.

Miezi miwili iliyopita Mr Nice alikuwa talk of the town nchini Kenya baada ya uongozi wa Grandpa kuitisha mkutano na vyombo vyote vya habari kwaajili ya kumtambulisha rasmi, na habari zake kuenea Kenya nzima kwa muda mfupi juu ya coming back yake kama msanii mkubwa na anaye heshimika.

Hakika hii ilikuwa ni nafasi nzuri sana kwa Nice kurudisha heshima yake katika muziki kutokana na jinsi alivyopokelewa kwa hadhi ya juu sana Kenya, ambapo Kabla hajaenda Nice alikuwa na mkataba na Lamar wa studio ya Fish Crab ambao walifanikiwa kutoa takribani nyimbo mbili ambazo hata hivyo hazikufanikiwa sana kumrudisha Yule mr. Nice wa Kidali Po, Fagilia, na zingine.

Hii ndio taarifa iliyotolewa na studio hiyo ya Grandpa ya Kenya kwa mashabiki kuhusu kusitisha kufanya kazi na Mr. Nice:

“To Grandpa Records fans and friends we’ve decided to drop Mr nice from Grandpa Records artists’ roster. Mr Nice has been terminated for violating the agreement we entered with him. For the sake of media and the general public we will summarize and say this, Mr Nice is the most difficult, uncooperative, lazy, unreliable artist we’ve ever worked with. The points and incidents of conflict are too many to mention here. To be brief Mr Nice had previously signed a deal with Sallam Sharaf and Lamar in Tanzania and did not disclose this to us at the point of being signed to grandpa records. All in all, aluta continua we tried our best but he failed us.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents