Habari

Mambosasa athibitisha ofisi ya DPP kuibiwa kompyuta ilizokuwa na nyaraka za kesi za uhujumu uchumi

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha tukio la kuibwa kwa kompyuta za Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) zilizokuwa na nyaraka za kesi za uhujumu uchumi.

Kamanda Mambosasa ameeleza kuwa jeshi hilo lilipokea taarifa hizo Jumanne, Oktoba 15, 2019 na linaendelea na uchunguzi.

“Ni kweli tukio hilo limetokea na polisi tumepokea taarifa Jumanne asubuhi, mpaka sasa hakuna mtu anayeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo,” Kamanda Mambosasa anakaririwa na Gazeti la Nipashe.

Hata hivyo, hakueleza idadi ya kompyuta zilizoibwa. DPP alipotafutwa hakuweza kuzungumza akieleza kuwa yuko kwenye kikao.

DPP amekuwa katika mchakato wa kupokea barua za watu wanaokiri kuhujumu uchumi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents