Burudani

Mamia waandamana kupinga show ya Pharrell Williams jijini Cape Town

Takriban watu 2000 waliandamana jana Jumatatu nje ya ukumbi uliopo jijini Cape Town, Afrika Kusini ambako Pharrell Williams alitumbuiza.

pharrell

Watu hao waliandamana kutokana na deal la matangazo la staa huyo na kampuni ya nchini humo, Woolworths yenye uhusiano wa kibiashara na Israel.

Hata hivyo waandamanaji hao waliondoka na Pharrell ametumbuiza kwenye ukumbi wa GrandWest Casino.

Muimbaji na mtayarishaji huyo wa muziki alikuwa amepangwa kutumbuiza licha ya maandamano hayo yaliyoanzishwa na shirika liitwalo Boycott, Divestment and Sanctions.

Watu hao wanaamini kuwa kwa kufanya kazi na Woolworths, Pharrell anaiunga mkono Israel, nchi ambayo inaionea Palestina.

Maandano yoyote yanayoiunga mkono Palestina huvutia waislamu wengi husasan katika mji wa Cape Town wenye waumini wengi wa dini hiyo.

Waandamaji hao walikuwa na mabango yaliyoandikwa: Pharrell is welcome if Gaza is free’ na ‘Pharrell and Woolworths have blood on their hands’.

Williams anatarajiwa pia kutumbuiza jijini Johannesburg, Alhamis hii.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents