Habari

Mamia wafariki kwenye mlipuko mkubwa wa Lebanon, chaelezwa kilichotokea

Lebanon inaomboleza vifo vya watu 78 vilivyotokea baada ya mlipuko mkubwa kutokea Sikh ya jana katika mji mkuu wa Beirut na kuwajeruhi wengine 4000.

Mji wote uliyumbishwa na mlipuko huo, ulioanza kwa moto katika bandari kabla mlipuko huo uliofanana na wingu la uyoga kutokea.

Rais wa Lebanon, Michel Aoun jana alisema kwamba tani 2,750 za ammonium nitrate zilikuwa zimewekwa vibaya katika ghala moja kwa miaka sita.

Aliitisha kikao cha dharura siku ya Jumatano , na kusema hali ya dharura ya wiki mbili imetangazwa.

Rais Aoun pia alitangaza kwamba serikali itatoa $66m za hazina ya dharura. ”Kile tunachoshuhudia ni janga kubwa” , alisema mkuu wa kundi la msalaba mwekundu George Kettani akizungumza na vyombo vya habari. ”Kuna waathiriwa kila mahali”.

Maafisa walisema siku ya Jumanne kwamba uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo kilichosababisha mlipuko huo.

Baraza kuu la ulinzi nchini Lebanon lilisema kuwa wale waliohusika wataadhibiwa vilivyo.

Ammonium Nitrate ilikuwa imeshushwa kutoka kwa meli iliokamatwa katika bandari hiyo 2013 na kuwekwa katika ghala.

Mlipuko huo unajiri wakati mgumu kwa upande wa taifa hilo , huku likikabiliwa na mgogoro wa kiuchumi unaosababishwa na mgawanyiko wa jadi huku taifa hilo likiathiriwa na mgogoro mwengine wa virusi vya corona.

Hali ya wasiwasi pia iko juu kabla ya uamuzi wa siku ya Ijumaa kuhusu kesi ya mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu Rafik Hariri 2005.

Je ni nini kilichotokea?

Mlipuko huo ulitokea muda mfupi baada ya mwendo wa saa kumi na mbili siku ya Jumanne.

Mwandishi wa BBC aliyekuwa katika eneo hilo aliripoti miili ya watu waliokuwa wameuawa na uharibifu mkubwa, unaoweza kuifunga bandari hiyo ya Beirut kwa muda.

Vyombo vya habari viliwaonyesha watu wakiwa wamenasa chini ya vifusi.

https://www.youtube.com/watch?v=8dbf3IAwQYk

Shahidi mmoja alielezea mlipuko huo kuwa mkubwa hali ya kwamba unaweza kusababisha watu kuwa viziwi, huku kanda ya video ikionesha magari yalioathirika pakubwa mbali na majumba yalioharibika. #prayforlebanon #prayforbeirut

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents