Burudani

Mamia wafurika kuangalia #Furious7 kwa mara ya kwanza kwenye majumba ya sinema Dar tiketi zaisha

Filamu ya Fast & Furious 7 imezinduliwa leo April 3 duniani kote.

Fast-Furious-7-9667

Tanzania ni moja ya nchi zilizoionesha filamu hiyo kwa mara ya kwanza.

Hamu kubwa ya mashabiki wa filamu nchini, imeyafanya majumba ya sinema jijini Dar es Salaam kuuza tiketi nyingi kuliko kawaida. Meneja wa Century Cinemax iliyopo Mlimani City jijini Dar es Salaam, Haji Madoweka, ameiambia Bongo5 Ijumaa hii kuwa tiketi za kuangalia filamu hiyo zimeisha kwa siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili.

Madoweka amedai kuwa filamu hiyo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wake na ndio maana tiketi zimeisha mapema kiasi cha kumfanya aongeze chumba kingine kwaajili ya kuwaruhusu watu wengine kuitazama.

Amesema kwa siku huonesha filamu mpya mara tano katika muda unaoanzia saa mbili asubuhi hadi saa saa nne usiku, lakini kutokana na watu wengi kununua tiketi, imewalazimu kuongeza show nyingine ya saa tano usiku.

“Kwa kawaida huwa hatuwezi kujaza siti zote lakini filamu hii imetufanya tuongeze show moja tena ya kuanzisha saa tano usiku,” amesema Madoweka. “Hapa ili kupata nafasi nzuri labda kuanzia Jumatatu.

Amedai kuwa kifo cha Paul Walker, kilichotokea November mwaka 2013 ni sababu moja wapo iliyoifanya Furious 7 ivutie watu wengi wanaotaka kujua alichomalizia kuigiza kabla mauti hayajamkuta.

Sam ni mmoja wa mashabiki wa filamu hiyo ambaye ameiambia Bongo5 kuwa alinunua tiketi mapema zaidi ili kuitazama Ijumaa hii. “Naipenda Fast and Furious sababu ya yale mashindano ya magari, napenda sana driving,” amesema Sam.

“Kingine nataka kufahamu Paul Walker alivyoigiza.”

Kwa upande wake Janet Loveness aliyeshindwa kuitazama filamu hiyo leo baada ya kukosa tiketi amedai ni Vin Diesel ndiye anayemvutia kwenye filamu hiyo. “Napenda uigizaji wa Vin Diesel, nataka kujua alichofanya kwenye Furious 7,” Janet ameiambia Bongo5.

Pamoja na kufariki kwa muigizaji wake muhimu Paul Walker mwaka juzi, filamu ya Fast & Furious 7 inatarajiwa kuingiza makadirio ya faida ifikayo dola bilioni 1.37.

Furious 7 inaweza kuingiza dola milioni 119 za mauzo ya tiketi katika weekend yake ya kwanza na dola milioni 283 kwenye majumba ya sinema nchini Marekani na Canada kwa mujibu wa BoxOffice.com.

Hiyo itafanya Fast & Furious kuwa filamu ya mfululizo hiyo yenye mafanikio zaidi kuliko zote. Kwa pamoja filamu za kwanza sita ziliingiza dola bilioni 2.38.

Walker alifariki akiwa na umri wa miaka 40 kwa ajali mbaya ya gari November 2013.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents