Burudani

Mamlaka ya elimu Tanzania kuandaa mbio za hisani kuchangisha fedha za ujenzi wa mabweni


Baada ya mamlaka ya elimu Tanzania, TEA, kuzindua kampeni ya CHANGIA TOFALI juzi kwenye hoteli ya Serena, sasa inajiandaa kufanya mbio za hisani jijini Dar es Salaam.
Akiongea na kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC 1 leo asubuhi, mratibu wa mabalozi wa kampeni hiyo, Receca Gyumi amesema anategemea watu wengi watajitokeza kwenye mbio hizo na kuchangia chochote walichonacho ili kusaidia ujenzi wa mabweni.
Rebeca amesema pia mabalozi hao wanategemea kufanya maongezi na spika wa bunge na wangependa kwenda bungeni kuongea na wabunge uso kwa uso.
Ameongeza kuwa katika ziara hiyo wasingependa ahadi kutoka kwa wabunge hao bali watawataka wachangie kiasi chochote kitakachokuwa kimebaki kwenye mifuko yao.
Akizungumzia kampeni ya CHANGIA TOFALI, mtangazaji wa kituo cha Channel O, Jokate Mwegelo ambaye ni mmoja wa mabalozi wa TEA, amesema jukumu la kusaidia ujenzi wa mabweni ni jukumu la kila mwananchi.
Kampeni ya CHANGIA TOFALI inawaomba wananchi kuchangia shilingi 250 pekee.
Mabalozi wengine wa TEA ni pamoja na Nancy Sumary (Miss Tanzania 2005), Faraja Nyalandu (Miss Tanzania 2004) na Mariam Ndaba (mwanamitindo na mmiliki wa blog).
Kikundi cha mabalozi hao watano, kimedhamiria kukusanya shilingi bilioni 2.3 zitakazotumika kujenga hosteli 30 za wasichana katika shule 1,504 nchini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents