Habari

Mamlaka ya hali ya hewa Kenya yadai mvua aliyotakiwa kunyesha nchini humo imekwama Tanzania

Idara ya hali ya anga nchini Kenya inasema kuwa kiangazi kitaendelea hadi mwisho wa mwezi huu huku upepo wa mvua ukisalia nchini Tanzania kutokana na kiwango cha chini cha upepo.

Mvua ndefu itaanza kunyesha katika maeneo mengi ya Kenya ifikiapo miwsho wa mwezi huu, wataalam wa hali ya anga wamesema.

Kaimu mkurugenzi wa shirika la hali ya anga nchini Kenya Stella Aura alielezea kwamba upepo wenye mvua umekwama nchini Tanzania kutokana na shinikizo ya kiwango cha chini ambayo haiwezi kuisukuma mvua hiyo kuelekea kaskazini mwa Kenya.

Mwezi Aprili ndio mwezi wa mvua ndefu nchini Kenya na onyo limetolewa katika maeneo kadhaa ya Kenya kuhusu kuchelewa kwake.

”Mvua ya msimu husababishwa na upepo wa mvua unaoelekea kaskazini lakini kufikia sasa upepeo huo haujaelekea kaskazini”, aliambia vyomb vya habari.”Mvua imekwama nchini Tanzania, mifumo ya upepo iliopo kusini haijashikamana kuweza kusukuma mawingu hivyobasi mvua itachelewa , lakini mvua itaanza kunyesha mwisho wa mwezi huu”, alisema.

Source: BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents