Michezo

Man City kukutana na Liverpool fainali ya kombe la Capital One

Klabu ya Man City imefanikiwa kufuzu kuingia fainali ya mchezo wa kombe la Capital One baada ya kuichapa Everton kwa mabao 3-1.

30A475C500000578-0-image-a-28_1453929946047

Everton ndio ilikuwa timu ya kwanza kupata goli baada ya kiungo Ross Barkley kuifungia timu yake bao la kuongoza katika dakika ya 18 ya mchezo.

30A43BAA00000578-0-image-a-10_1453926629326

Kiungo kutoka Brazil Fernandinho akasawazisha bao hilo kwa shuti kali baada ya kutokea piga nikupige kwenye goli la everton katika dakika ya 25.

Kevin De Bruyne akaongeza bao la pili baada ya kuunganisha krosi ya kutoka upande wa kushoto iliyopigwa na Raheem Sterling, kisha Sergio Aguero kun, akahitimisha kazi kwa bao la tatu.

Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Goodson Park Everton walishindwa kwa ushindi wa mabao 2-1. Man City watachuana na Liverpool katika mchezo wa fainali utaofanyika Februari 28 katika dimba la Wembley.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents