Michezo

Man City yakaribia kumnasa kipa wa Benfica, Ederson Moraes

Manchester City wanakaribia kumnunua kipa wa mabingwa wa ligi ya Ureno Benfica, Ederson Moraes, kwa jumla ya £33m.  Meneja wa City Pep Guardiola, amekuwa akimtafuta mchezaji huyo wa Brazil kwa muda na sasa amepata nafasi baada ya kumwachilia kipa wa klabu hiyo Willy Caballero siku ya Ijumaa.

Ederso, alisaidia Benfica kushinda kombe la ligi ya Ureno mara 26 siku ya Jumapili dhdid ya klabu ya Vitoria Guimaraes 2-1.

Baada ya ushindi wa 2-1 katika fainali ya Kombe la Ligi nchini Ureno, Moraes alisema kuwa kuna uwezekano hiyo ikawa ni mechi yake ya mwisho kuichezea benfica.

Taarifa zinasema Guardiola pia anataka kumnunua beki wa kati Mfaransa anayechezea Monaco Benjamin Mendy, 22.

Baada ya kushindwa kunyakuwa kombe lolote katika msimu wake wa kwanza  akiwa katika klabu ya Manchester City , Guardiola amepanga kufanyia mabadiliko makubwa ndani ya kikosi cha klabu hiyo kabla ya msimu ujao kuanza.

Pep, alichukua hatua ya kwanza kwa kumnunua kiungo wa Monaco, Mreno Bernardo Silva kwa £43m juma lililopia.

Caballero ni miongoni mwa wachezaji watano wa City ambao mikataba yao imefikia kikomo na wameruhusiwa kuondoka.

Hatima ya wachezaji wanne ambao Guardiola aliwaruhusu waondoke ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake Etihad, kwa mkopo msimu uliopita – Joe Hart, Samir Nasri, Wilfried Bony na Eliaquim Mangala – bado haijabainika.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents