Burudani ya Michezo Live

Man Fongo na Mesen Selekta sasa ni paka na chui

Producer wa De Fatality Music, Mesen Selekta na mkali wa muziki wa Singeli Man Fongo kwa sasa ni kama paka na chui.

Selekta ndiye producer wa nyimbo nyingi za Fongo ukiwemo uliompa umaarufu, Hakuna Ushemeji. Sababu za wawili hao kugeuka maadui ni pesa kwa mujibu wa Man Fongo japo Selekta amezunguka mbuvu kuitaja.

“Ni kweli kuna tofauti ambayo ipo mimi na Man Fongo,” Mesen alikiambia kipindi cha Twenzetu cha Times FM.

“Naweza kusema ni kutokuwa na maelewano mazuri kati ya yeye Man Fongo pamoja na studio ya De Fatality kwa ujumla ndio kilichosabisha tofauti,” aliongeza.

Hata hivyo Man Fongo alielezea mkasa mzima wa kilichosababisha kuvunjika kwa ukaribu wao kuwa ni Mesen alipata deal ya shilingi milioni 10 la Man Fongo kutengeneza tangazo la Tigo lakini akamuambia kuwa ni la milioni 2.5 na kwamba atamlipa laki mbili na nusu na fedha zingine watumie kurekebisha studio yao.

Fongo amesema baada ya kugundua mchezo huo, alikataa kufanya tangazo hilo na kumwacha Mesen njia panda. “Mpaka leo Mesen hataki kuniona hata kunisikia, yaani ananichukia we acha,” alisema Man Fongo.

“Mimi hata kukaa naye kuzungumza naye sitoweza kwasababu kwanza namuona snitch sio mtu mzuri, ina maana milioni 10 yote inatoka anataka kupata hela yeye, ina maana mimi na yeye nani msanii anayeimba?”

“Kataka kutumia yeye, yaani anatumie mgongo wangu mimi nimtengenezee tangazo halafu achukue milioni 10, hivyo ndio tunaishi kweli? Katika milioni 10 mimi nipate laki mbili? Ahh uongo mbali, sio kweli.”

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW