Michezo

Man U yarejea Kileleni

manchester-united

 

Timu ya Man United usiku wa kuamkia jana waliweza kurejea kileleni mwa ligi hiyo baada ya kuifunga timu ya Arsenal goli moja kwa bila. Goli hilo lilifungwa na Ji-Sung Park dakika ya 41 ya mchezo.

Man United ilionekana kumiliki mpira kwa kipindi cha kwanza huku kiungo Mbrazil Andason akionyesha kiwango cha hali ya juu na kuifanya timu hiyo kuwa kwenye kiwango cha hali ya juu kwa kipindi hicho cha kwanza. Kipindi cha pili kilikuwa cha Arsenal kwani watoto wa Wenger walirudi na kutulia na kufanya kile walichotakiwa kukifanya lakini bahati haikuwa yao kwani waliwaingiza Cesc Fabregas Theo Walcot na Van Persie ambao walileta mabadiliko makubwa ya kufanya Man United kuzuia kwa muda kulinda goli lao.

Wayne Rooney hakuonyesha sana kasi yake ambayo wapenzi wa soka wanaijua kwani alikuwa amepooza sana kiasi cha kuzibitiwa na mabeki wa Arsenal vizuri. Mchezaji huyo alipewa penalty ambayo ilisababishwa na beki wa kushoto wa Arsenal Gael Clichy baada ya kuunawa mpira eneo la hatari, lakini bado rooney alikosa shuti hilo.

Sasa Man United wanarejea kileleni mwa ligi hiyo na kuwa na Point 34 huku Arsenal ikiwa inashika nafasi ya pili ikiwa na point 32. Man United ikiwa inaongoza ligi bado wana mchezo mmoja mkononi ambao iliahiriswa baada ya kuwepo na barafu uwanjani wiki ilio pita,ambao haijajulikana lini watacheza mchezo huo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents