Burudani ya Michezo Live

Man United kumng’oa mshambuliaji wa Juve, Liverpool na Napoli zatunishiana misuli kuwania saini ya mchezaji huyu wa KRC Genk

Liverpool na Napoli ni miongoni mwa klabu zinazomfuatilia kwa karibu kiungo wa kati wa Genk raia wa Norway, Sander Berge 21, kwa mujibu wa mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo, Dimitri de Conde. (Radio Punto Nuovo, via Goal)

Image result for Sander Berge genk

Napoli huenda ikampoteza mchezaji wa kimataifa wa Albania Elseid Hysaj, 25, bila chochote mkataba wake utakapokapomalizika msimu ujao, lakini ingelipokea £43m kutoka kwa Chelsea msimu uliopita, anasema wakala wake Mario Giuffredi. (Radio Punto Nuovo via Mail)Frank LampardFrank Lampard ameiongoza Chelsea kushinda mara 8 katika mechi 10 ya mashindano yote yaliopita

United inatarajia kuafikiana na Juventus kuhusu usajili wa mshambuliaji wa Croatia Mario Mandzukic, 33, kufanya mazoezi na klabu hiyo mwezi ujao kabla ya uhamisho wa Januari. (Tuttosport – in Italian)Mshambuliaji wa Croatia Mario Mandzukic

Mandzukic ameichezea Croatia mara 89 tangu alipojiunga na tinmu ya taifa mwaka 2007

Mandzukic pia analengwa na klabu za ligi kuu ya soka. (Calciomercato)

Kocha wa Inter Milan Antonio Conte anataka kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud, 33, kutoka ndani ya klabu yake ya zamani,Chelsea. (Express)

Olivier Giroud

Manchester United ina nafasi nzuri ya kumsajili mshambuliaji wa Red Bull Salzburg na Norway Erling Braut Haaland, 19, ambaye alifunzwa na Ole Gunnar Solskjaer akiwa Molde. (Dagbladet – in Norwegian)

Newcastle inataka kusaini mkataba na mchezaji wa safu ya kati wa Arsenal na Switzerland Granit Xhaka, 27, kwa mkopo mwezi Januari. (Telegraph)

AC Milan ina mpango wa kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Uswiss ambaye kwa sasa hana klabu Zlatan Ibrahimovic, 38, mwezi Januari dirisha la uhamisho litakapofunguliwa, lakini mpango huo unahitaji kuidhinishwa na afisa mkuu mtendaji Ivan Gazidis. (Calciomercato)Zlatan Ibrahimovic,AC Milan ina mpango wa kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Uswiss, Zlatan Ibrahimovic, 38

Wakala wa beki wa Arsenal Mhispania Hector Bellerin anasema mteja wake, 24, haoni “jinsi msimu utakavyoenda”katika uwanja wa Emirates baada ya kupokea ombi la usajili kutoka Italia. (Sky Sport Italia via Football Italia)

Frank Lampard atajaribu tena kumjumuisha Shay Given katika kikosi cha wakufunzi wa Chelsea licha ya hofu kuhusu kipa huyo wa Uhispania Kepa Arrizabalaga, 25. (Mail)

Meneja wa Aston Villa Dean Smith ameidhinisha kuuzwa kwa kipa wa Croatia Lovre Kalinic, 29, mwezi Januari. (Football Insider)

Mashabiki 114 wa Manchester City waliosafiri kwenda Kharkiv kushangilia mechi ya Champions League kati ya klabu hiyo na Shakhtar Donetsk msimu huu wametambuliwa rasmi kwa barua ya kibinafsi kutoka kwa Pep Guardiola. (Manchester Evening News)Pep GuardiolaManchester City ilishinda taji la ligi kuu ya Premia kwa alama 100 chini ya uongozi wa Pep Guardiola msimu uliopita

Manchester United inatarajia kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 26, atarejea uwanjani kushiriki mechi ya Manchester City Disemba 7. (Sun)

Mshambuliaji mwingine wa zamani wa Chelsea striker, Didier Drogba, 41, anasema alipewa nafasi ”nzuri” ya ukufunzi katika klabu hiyo lakini alikataa kurejea Stamford Bridge ilikufuatilia azma yake ya kuwania nafasi ya urais wa shirikisho la soka la Ivory Coast FA. (Metro)

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW