Michezo

Man United, Liverpool, Man City hati hati kuvaana na Barcelona hatua ya 16 bora ya UEFA

Klabu za Liverpool, Man United na Man City vipo katika nafasi kubwa kupangiwa na Mabingwa wa Hispania FC Barcelona kwenye hatua ya 16 bora ya klabu bingwa barani Ulaya.

Katika hatua hiyo Barcelona haitakutana na klabu yoyote kutoka Hispania, wala na Spurs ambao wote walikuwa kundi B kwenye hatua ya makundi.

Klabu nyingine ambazo zinaweza kupangiwa na Barcelona ni AS Roma, Juventus, Ajax, Bayern Munich au Lyon.

Droo ya 16 bora itachezwa Jumatatu ijayo Desemba 17 mjini Nyon nchini Uswisi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents