Michezo

Man United wafikia makubaliano na juventus kumsajili Mandzukic, Rakitic athibitisha kuikimbia Barcelona

Man United wafikia makubaliano na juventus kumsajili Mandzukic, Rakitic athibitisha kuikimbia Barcelona

Manchester United wameafikiana makubaliano ya maongezi ya kumsajili mwezi Januari mshambuliaji wa Croatia na klabu ya Juventus Mario Mandzukic, 33. (Tuttosport, via Mirror)

Lyon wameshindwa mipango yao ya kumsajili kocha wa zamani wa Chelsea na Manchester United Jose Mourinho. Kocha huyo mwenye mika 56 raia wa Ureno anataka kurejea kwenye ligi ya Primia ya England. (Mirror)

Klabu ya Fenerbahce ya Uturuki inaaminika kuanza mazungumzo na Arsenal juu ya kumsajili kwa mkopo mwezi Januari kiungo Mesut Ozil, 30. (Takvim, via Sun)

Ozil ana wasi wasi kuwa hatacheza tena katika klabu ya Arsenal. (Mirror)

Mshambuliaji wa Ujerumani Thomas Muller, 30, hana furaha baada ya kupunguziwa muda wa kucheza katika klabu yake ya Bayern Munich na amekiri kuwa anaweza kusaka timu ya kuhamia mwezia Januari. (Kicker, via Mail)

Mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 32, na beki wa Brazil Thiago Silva, 35, wanaweza kuondoka bure kutoka klabu ya Paris St-Germain mwishoni mwa msimu. (ESPN)

Cavani

Kiungo wa Barcelona na Croatia Ivan Rakitic, 31, ambaye alikuwa akihusishwa na uhamisho kwenda Manchester United msimu uliopita, amesema kuwa huenda akaihama klabu yake ili kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza. (Mail)

Leeds wanapanga kumsajili kocha wa Rangers ya Uskochi Steven Gerrard endapo kocha wao Marcelo Bielsaataihama klabu. (Football Insider)

Manchester United wanapanga kumsajili kiungo Francisco Sebastian Cordova, ambaye anachezea klabu ya America ya Ligi Kuu nchini Mexico. Kiungo huyo mwenye miaka 22 ambaye ameichezea timu ya taifa lake kwa mara ya kwanza juma lililopita pia anatakiwa na Sevilla na Benfica. (Mail)

CordovaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Mcezaji mmoja mwandamizi wa Manchester United aliandaa mlo katika moja ya mgahawa kwa kikosi kizima lakini ni wachezaji watano tu ndio waliokwenda.. (ESPN)

Juventus na Napoli wanamnyemelea mshambuliaji kinda wa klabu ya Red Bull Salzburg na timu ya taifa ya Norway striker Erling Haaland, 19, ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa vilabu vya Nottingham Forest, Leeds na Manchester City Alf-Inge Haaland. (Corriere dello Sport – in Italian)

Sergei Gnabri

Kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger anaamini Bayern Munich “walimlaghai” mshambuliaji wa Ujerumani Serge Gnabry, 24, ili kuihama Arsenal mwaka 2016. (Goal.com)

Mlinzi wa England Harry Maguire, 26, anaamini usajili wake wa pauni milioni 80 ulikuwa ni “dili nzuri” baina ya vilabu vya Manchester United na Leicester. (Leicester Mercury)

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents