Michezo

Man United waichinja Chelsea, Old Trafford

Klabu ya Manchester United imefanikiwa kurudi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu England (EPL) kwa kuitafuna klabu ya Chelsea goli 2-1.

Lukaku na Jesse Lingard

Chelsea walikuwa ndio wa kwanza kuliona langu la United kupitia kwa Wilian kunako dakika 32 kabla ya Romelu Lukaku kusawazisha kunako dakika ya 39 na hadi mapumziko timu zote zilikuwa 1-1.

Goli la ushindi la United limefungwa na kinda, Jesse Lingard kunako dakika ya 75 hadi filimbi ya mwisho inalia, Man United 2 Chelsea 1.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents