Michezo

Man United yaifuata CSKA Moscow bila ya Fellaini

Mchezaji wa Manchester United, Marouane Fellaini hatokuwepo katika mchezo wa Klabu bingwa barani Ulaya wakati timu yake itakapocheza dhidi ya CSKA Moscow siku ya Jumatano ya wiki hii huko nchini Urusi.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji hayumo kwenye kikosi cha Manchester ambacho kimeondoka mchana waleo kuelekea Urusi, baada ya kushindwa kupona jeraha lake la mguu alilopata katika mchezo wa Jumamosi wa Ligi Kuu dhidi ya Southampton.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake Old Trafford kinaeleza kuwa mpaka sasa haijafamika kuwa Fellaini  atachukuwa muda gani kurejea katika uwanjani.

United itashuka dimbani siku ya Jumatano kuvaana na watukutu wa Urusi klabu ya CSKA Moscow katika mchezo wa Klabu bingwa barani Ulaya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents