Tia Kitu. Pata Vituuz!

Man United yatabiriwa kushuka daraja, hatma ya Ole Gunnar Solskjaer kujulikana baada ya mechi dhidi ya Norwich

Kuna uwezekano Manchester United ikashuka daraja msimu huu, kwa mujibu wa kocha wa zamani wa England, Sam Allardyce. (Talksport)

Image result for ole gunnar solskjaer in bad moment

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer atafutwa kazi endapo timu yake itafungwa na Norwich mwishoni mwa mwezi, ripoti zinaeleza. (Sun)

Hata hivyo, vyanzo vingine vinaarifu kuwa uongozi Man United upo tayari kumvumilia na kumpa muda zaidi Solskjaer wa kufanya mageuzi klabuni, licha ya kiwango kibovu cha matokeo ya mwanzo wa msimu kwa miaka 30. (Telegraph)

United wanapanga kuwasajili kiungo wa West Ham na England Declan Rice, 20, na beki wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly, 28, bila kujali mustakabali wa Solskjaer. (Goal)Kalidou Koulibaly

Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino napanga kuwauza wachezaji kadhaa wa klabu hiyo baada ya kuanza msimu kwa kiwango kibovu. Wachezaji watakaowekwa sokoni mwezi Januari ni; Eric Dier, 25, Christian Eriksen, 27, Serge Aurier, 26, Victor Wanyama, 28, pamoja na Danny Rose, 29. (Times – subscription required)

Kocha David Moyes yupo tayari kurudi kuifunza klabu yake ya zamani ya Everton, katika kipindi ambaco kocha wa sasa Marco Silva akiwa katika shinikizo kubwa baada ya timu hiyo kuwa chini ya mstari wa kushuka daraja. (Mirror)

Crystal Palace watalazimika kulipa pauni milioni ili 22 wamsajili mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya Ubelgiji Michy Batshuayi, 26, ambaye yupo kwa mkopo Palace toka Januari mwaka huu. (Express)Michy Batshuayi,

Kiungo wa Arsenal Dani Ceballos, 23, amesema alaifanya uamuzi sahihi kujiunga na ‘the Gunners’ kwa mkopo akitokea Real Madrid baada ya kuitwa tena kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uhispania. (Goal)

Klabu ya Barcelona itampatia kipa wake Mjerumani Marc-Andre ter Stegen, 27, mkataba wa muda mrefu hivi karibuni. (Marca)

Mshambuliaji wa zamani wa Sunderland Kevin Phillips anataka kuchukua nafasi ya ukocha wa timu hiyo baada kufutwa kazi kwa kocha Jack Ross. (Star)

Borussia Dortmund wameungana na Arsenal, Juventus na Paris St-Germain katika kufuatilia maendeleo ya winga kinda wa Celtic ya Uskochi, Karamoko Dembele, mwenye miaka 16. (Bild – in German)Karamoko Dembele

Mshambuliaji raia wa Argentina Paulo Dybala, 25, amesema hakuwa na mpango wa kuondoka Juventus msimu huu licha ya kuhusishwa na uhamisho kuelekea vilabu vya Manchester United na Tottenham. (Tuttosport – in Italian)

Lyon inatarajiwa kufanya mazungumzo na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa na Paris St-Germain Laurent Blanc baada ya kumtimua kazi Sylvinho. (L’Equipe – in French)

Beki wa kati wa Arsenal na Ujerumani Shkodran Mustafi, 27, amekasirishwa vikali na kura ya maoni iliyoendeshwa na gazeti la Uhispania la Marca ambapo ametajwa kuwa beki namba mbili mbovu zaidi duniani baada ya Phil Jones wa Man United.Beki wa kati wa Arsenal na Ujerumani Shkodran Mustafi,

Ushiriki wa klabu za Ligi ya Primia ya England katika michuano ya Champions League utapunguzwa kutoka timu nne zinazofuzu moja kwa moja mpaka timu tatu, chini ya mapendekezo mapya ya kanuni za mashindano. (Mail)

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW