Michezo

Man United yatangaza mapato yake ya mwaka 2017

Manchester  United imeripoti mapato ya paundi milioni 581 katika kipindi cha fedha cha mwaka 2017 huku mapato ya haki za matangazo yakiongezeka.

Baada ya ushindi wake wa kombe la Europa  na EFL  United imetia saini kandarasi 12 za ufadhili huku mapato ya matangazo pamoja na yale yanaopatikana wakati wa mechi yakiongezeka.

Manchester United ilifaidika kutoka kwa ongezeko la mapato ya runinga wakati wa kipindi cha mwaka 2016/17  huku ukiwa ndiyomwaka wa kwanza kati ya mitatu ya makubaliano ya matangazo ya runinga.

Juni 30, mapato ya matangazo yaliongezeka hadi kufikia paundi milioni 194 kutoka 140 iliyokuwa hapo awali ikiwa nisawa na ongezeko la silimia 38.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents