Burudani ya Michezo Live

Man Walter kumleta tena 20 Percent baada ya kumaliza tofauti zao

Mshindi wa kipengele cha mtayarishaji bora wa Bongo Flava wa KTMA 2013, Man Walter amemaliza tofauti yake na 20 Percent na anatarajia kumleta tena kwenye chart.

e703f2962c2511e3892122000a9f13f9_7
Peace… (Picha: Salma Msangi Instagram)

Kwa muda mrefu mtayarishaji huyo wa hit ya Lady Jaydee, Yahaya, hajafanya kazi na 20 ambaye aliwahi kuibuka na tuzo kibao miaka iliyopita. Akiongea Kali za Bomba ya Bomba FM, Man Walter alisema tayari wamekaa na 20 Percent katika mazungumzo rasmi ya kumrudisha tena na hawana tena tofauti.

“Vitu vingi watarajie kutoka kwangu sababu ukimya huo uliopo ni kwasababu ya kuwaandalia vitu vizuri,” alisema 20 Percent.

Sikiliza zaidi interview hiyo hapa.

[soundcloud url=”http://api.soundcloud.com/tracks/113642150″ params=”” width=” 100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Kwenye ukurasa wa Facebook wa Magic FM wameandika:

Man Water na Twenty Percent walikutana leo katika studio za Magic fm na Channel ten ambapo wawili hao wamekubaliana kufanya kazi tena pamoja na kusahau yaliyopita.

Akizungumzia kiundani kuhusu tofauti zao Man Water alisema tatizo lilikua ni kutoelewana au kupishana kwa kauli ambazo leo walizimaliza na hatimaye kuweka mikakati mipya ikiwemo ya kufanya kazi pamoja kwa makubaliano maalumu.

Kwa upande wake 20% amesema tofauti zao hazikuwa za msingi bali ni kupishana tu kwa kauli na sasa yuko tayari kufanya kazi pamoja na Man Water.

Inaaminika kwamba kufanya kazi pamoja kwa wawili hao kunaleta mwamko mkubwa kwa washabiki wao kutokana na kuelewana katika kazi zao mbalimbali walizowahi kufanya ikiwemo kaziya Yanini malumbano, Tamaambaya, Mama Neema na nyinginezo.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW