Michezo

Manara afunguka walichokubaliana Simba ”Hatuachi kikombe mwaka huu, tutaviokota vyote, hakuna kumuachia mtu”(+video)

Siku ya Jumamosi 17 Agosti, Mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC wanatarajia kuingia uwanjani kukakibiliana na Mabingwa wa Azam Federation Cup, Azam FC.

Kuelekea katika mchezo huo Wasemaji wa timu zote mbili wamezungumza na waandishi wa habari makao makuu ya shirikisho la soka Tanzania TFF.

Kwa upande wake afisa habari wa Azam Jaffar Idd Maganga amesema timu yao inaelekea kambini ili kuhakikisha natwaa taji hilo.

”Azam FC imeingia kambini kujiandaa na mchezo huu wa Simba, tutautumia zaidi kwaajili ya kufanya marekebisho. Hasa kwa kuangalia jinsi gani ya kuboresha kikosi, wachezaji wanauchukulia kwa umuhimu.”

”Simba mara ya mwisho wakati tunacheza nao waliihitaji ushindi zaidi lakini tukatoka sare ya bila kufungana, walishindwa kutufunga na kuzuka maneno mengi kwamba Azam tumewabania Simba, lakini mchezo wa mpira hauna’formula’ kila mmoja anaingia uwanjani ili kushinda na kuwapa furaha mashabiki wake. Tupo vizuri tunawasubiri”

Akizungumza, Haji Manara amesema ”Sisi Simba hatunamengi ila tunawaomba wafuasi wetu, hawa sisi hatuwaiti wachezaji wa 12, ni zaidi ya 12, 13 hawa ndiyo nyota wa mchezo, Simba haina staa zaidi ya mshabiki wake ndiyo ngao yetu na ndiyo kinga yetu na ndiyo dawa yetu.”

Haji Manara ameongeza ”Tumeshinda mara mbili mfululizo Ngao ya Hisani tunahihtaji kushinda tena mara ya tatu. Tunataka kuchukua Ngao za Hisani kwa miaka 10 mfululizo, kama ambavyo tutachukua ubingwa wa ligi kuu miaka 10 mfululizo hakuna kumuachia mtu. Kwa hiyo tunataka na Ngao za Hisani tuziokote.”

”Tumekubaliana ndani ya klabu, kwa wachezaji huu ni mwaka wa vikombe (trophies), hatuachii kikombe mwaka huu tumekubaliana kabisa, kila kikombe tutakachoshiriki tunataka kukichukua.”

 

”Tunajua tutakuwa na changamoto kubwa sana ubingwa wa Afrika, ndiyo maana klabu imeweka lengo ‘target’ yetu ni nusu fainali tukivuka hapo Alhamdulilah, lakini hivi vingine vya nyumbani hivi unachukua unaviweka ndani.”

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents