Michezo

Manara, Antonio Nugaz na Luc Aymael kufuatiliwa, kutofungua Mlango kwa mponza kocha wa Simba

Taarifa ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kwa Vyombo vya Habari leo Kimeielekeza Sekretarieti kufuatilia viongozi wa vilabu na Makocha ambao hivi karibuni wamekuwa wakishutumu na kutoa matamshi yenye kukashifu na kudhalilisha viongozi, Chapa (Brand) ya Ligi na Taasisi kwa ujumla kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii

 

”Kikao cha ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi kilichokaa Februari 10,2020 Kimeielekeza Sekretarieti kufuatilia viongozi wa vilabu na Makocha ambao hivi karibuni wamekuwa wakishutumu na kutoa matamshi yenye kukashifu na kudhalilisha viongozi, Chapa (Brand) ya Ligi na Taasisi kwa ujumla kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwa vipindi tofauti tofauti. Viongozi na Makocha waliobainika ni wafuatao Kocha wa Klabu ya Namungo FC(Hitimana )-kwenye mchezo wa Simba SC na Namungo Fc, Kocha wa Klabu ya Young African Sc (Luc Aymael)-kwenye mchezo wa Yanga Sc na Lipuli, Msemaji wa Klabu ya Simba SC (Haji Manara) na Muhamasishaji wa Young African sc(Anthonio Nugaz). Kutokana na matamshi hayo wanapelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF).” Imeandika Taarifa hiyo.

Mbali na hilo Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetoa onyo kali kwa kocha wa klabu ya Simba

”Kocha wa Simba Sven Vanden Broeck amepewa Onyo Kali kwa kosa la kugoma kuwafungulia mlango mwamuzi na Kamishina wa mchezo wakati wa ukaguzi wa timu katika mechi hiyo iliyochezwa Februari 01,2020 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni namba 41(13) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Makocha.Maamuzi ya Kikao cha Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi kilichokaa Februari 10,2020.”

”Klabu ya Polisi Tanzania imepigwa Faini ya kiasi cha Tsh.1,500,000/=(Milioni Moja na Laki Tano) kwa kosa la kutumia mlango usio rasmi wa kuingia Uwanjani katika mechi iliyochezwa Februari 04,2020 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.Adhabu hii imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(14) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.”

”Mwamuzi Abubakar Mturo amefungiwa miezi mitatu(3) kwa kosa la kushindwa kumudu mchezo katika mechi iliyochezwa Februari 05,2020 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni namba 39(1) ya Ligi Kuu Kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.”

”Mchezaji wa Klabu ya Azam Fc Agrrey Moris amepigwa Faini ya kiasi cha Tsh.200,000/=(Laki Mbili) kwa kosa la kugoma kuongea na waandishi wa habari mara baada ya mchezo kumalizika katika mechi iliyochezwa Februari 05,2020 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.Adhabu hii imetolewa kwa mujibu wa Kanuni namba 38(18) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.”

Taarifa hiyo ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetolewa leo siku ya Alhamisi kwa vyombo vya habari.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents