Burudani

Manara ataka Bongo Movie wapongezwe, Awapa somo wakitaka wafike mbali (video)

Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara amewataka Watanzania wawe wepesi wa kutoa pongezi pale wasanii wa filamu nchini Tanzania (Bongo Movie) wanapofanya vizuri, na sio kuwapeza na kuwaponda kila siku kwani kitendo hicho kinawakatisha tamaa waigizaji wetu.
https://youtu.be/U7Q7BxFW2RQ
Akizungumza wikiendi iliyopita kwenye sherehe za ugawaji wa tuzo za SZIFF, Manara amesema kuwa Tasnia ya Bongo Movie ni moja ya tasnia kubwa nchini Tanzania na wasanii wenyewe ndio waliyopigania kuifikisha hapa, hivyo ni wajibu wao kutaka kusonga mbele au kusalia hapa hapa.

Akitoa ushauri kwa waigizaji, Manara amewaomba wasanii wa Bongo Movie kama wanataka kufika mbali lazima wawe makini na wabunifu kwenye kazi zao na pia waache utoto na kutambua kuwa filamu ni kazi kama kazi nyingine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents