Michezo

Manara atuma salamu kwa Mwana FA ‘Engineer Mwana FA soma hiyo, Ferrari ndio hadhi ya msemaji mkubwa’

Ikiwa imepita siku moja tu ,tangu klabu ya Simba kupata matokeo mabaya ya kufungwa jumla ya mabao 3 – 2 dhidi ya Mashujaa FC na kuyaaga mashindo ya Azam Sports Federation Cup (FA), mapema hii leo Afisa habari wake, Haji Manara ameonyesha gari jipya aina ya Ferrari  huku akielezea kuwa msemaji mkubwa ndiye mwenye hadhi ya kutumia.

Kupitia ukurasa wake wakijamii wa Instagram, Manara ameweka picha ya gari jipya aina ya Ferrari huku akiandika gari hilo ndio hadhi ya msemaji mkubwa mwenye ustaa wake.

This image has an empty alt attribute; its file name is mamaaaa-600x359.jpg

”Engineer @mwanafa soma hyo!!, Yajayo ndio hayo madhee!!, Ferrari ndio hadhi ya msemaji mkubwa mwenye wastawa wakemjini!!, No Nzi wala lift,Dadadeki,” ameandika Manara kwenye mtando wake wa Instagram

Mkuu huyo wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC, Haji Manara ameonekana  kwenye gari hiyo ya Ferrari ya rangi nyekundu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents