Aisee DSTV!

Manara avunja ukimya kwa RC Makonda “Umewapa wale saba, sisi wakutunyima hata heka tatu tujidai, kufanya kote vizuri robo fainali Mabingwa Afrika, mbona Simba humtaji kwenye neema hii ya Ardhi, ” (+ Video)

Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara ameamua kuvunja ukimya na kumuomba Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda kuwapatia ardhi kama vile alivyofanya kwa wapinzani wao wa jadi Yanga SC.  Manara ameyasema hayo mbele ya mkutano wa Harambee ya kuichangia timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, bila kumungunya maneno aliamua kutumia nafasi hiyo kufikisha wazo lake kwa RC Makonda “Mhe. Binadamu tumeumbwa na wivu, na sisi Binadamu tumeumbwa na nyongo, kufanya kote vizuri huko robo fainali Mabingwa Afrika, mbona Simba humtaji kwenye neema hii ya Ardhi”

 

Kauli ya msemaji huyo inakuja ikiwa zimepita siku chache tu tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda kuwapatia uwanja klabu ya Yanga uliyopo Kigambo ikiwa kama mchango wake katika siku ya Kubwa Kuliko iliyoandaliwa na mabingwa hao wa kihistoria kama sehemu ya kukusanya michango kutoka kwa wadau mbalimbali wa michezo.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW