Habari

Manara na wenzake 18 warudi uraiani baada ya kukamatwa na polisi kufuatia kutekwa kwa Mo Dewji

Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara na wenzake 18 jana usiku wameachiwa kwa dhamana  baada ya kushikiliwa na polisi kwa siku nne wakihusishwa na tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji.

Image result for Haji manara
Haji Manara

Taarifa ya kuachiwa kwa watu hao imetolewa leo Jumanne Oktoba 16, 2018 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, ambapo amesema Watu 19 kati ya 26 waliokuwa wakishikiliwa na  polisi wakihusishwa na tukio la kutekwa mfanyabiashara Mo Dewji wameachiwa kwa dhamana huku upelelezi ukiendelea kufanyika.

Hata hivyo, Mambosasa amesema jeshi la polisi linaendelea kuwashikilia watu wengine saba waliohusishwa na tukio hilo.

Manara alikamatwa Oktoba 12, 2018 kutokana na kusambaza taarifa za tukio la kutekwa kwa Mo Dewji kwenye mitandao ya kijamii akidai katumwa na familia ya Mo jambo ambalo ilibainika sio la kweli.

Dewji alitekwa na watu wasiojulikana Alhamisi Oktoba 11, 2018 saa 11 alfajiri akienda mazoezini na hadi sasa hakuna taarifa rasmi ya nani aliyemteka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents