Manara: Senzo uje ofisini kukabidhi nyaraka zetu, Simba ni huge Club

Baada ya aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Masingiza raia wa Afrika Kusini kutangaza kujiuzulu ndani ya klabu hiyo siku ya jana huku kukiwa na tetesi kuwa huenda akajiunga na klabu ya Yanga na baada ya ujumbe wa Senzo klabu ya Simba haikuwa kimya na kutoa taarifa kuwa klabu hiyo haitahusika ni uamuzi au taarifa yeyote itakayotolewa na Senzo wakimaanisha hana mamlaka tena ndani ya Simba.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram wa msemaji wa klabu hiyo Haji Manara amepost ujumbe ukiambatana na picha yenye viongozi wa Yanga na Senzo ulioonyesha kuchukizwa na uamuzi wa Senzo akiandika kuwa” kwa hiyo mzunguko wa dunia umesimama siyo? Simba ni huge Club (klabu kubwa) our hope (matumaini yetu) kesho Senzo utakuja kukabidhi ofisi na nyaraka zetu kama utaratibu unavyosema. Kifuatacho.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW