Michezo

Manchester City hatiani kushiriki UEFA msimu ujao, kwa kukiuka baadhi ya vifungu vifuatavyo vya sheria ya fedha katika soka

Manchester City hatiani kushiriki UEFA msimu ujao kwa kukiuka baadhi ya vifungu vifuatavyo vya sheria ya fedha

Kamati ya Chama cha Soka Barani Ulaya(UEFA) inayoichunguza klabu ya Manchester City kwa kudaiwa kuvunja sheria ya fedha inatarajiwa kupendekeza Klabu hiyo kufungiwa msimu mmoja kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Ulaya iwapo itakutwa na hatia.


UEFA ilifungua uchunguzi huo baada ya kuwepo madai kuwa Mabingwa hao wapya wa Ligi Kuu England wamevunja vifungu kadhaa ya Sheria ya fedha iitwayo ‘Financial Fair Play – FFP’, lakini Klabu hiyo ilikana madai hayo na kusema ni uongo.

Sheria ya FFP ilitengenezwa ili kuhakikisha kuwa kiasi cha fedha kinachotolewa na klabu katika kumnunua mchezaji na katika mshahara kinaendana na kiasi klabu inapata katika matangazo na fedha za tuzo.
Aidha, huku taarifa ya UEFA ikisema haiwezi kuzungumzia suala hilo, Man. City imesisitiza kuwa haijafanya kosa na imewasilisha ushahidi wao mbele ya kamati ya uchunguzi.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents