Michezo

Manchester City kumkalisha nje Morata kwa zaidi ya mwezi 1

Mshambuliaji hatari wa klabu ya soka ya Chelsea ya Uingereza, Alvaro Morata anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha takribani wiki sita kwa kuuguza majereha.

Morata alipata majeraha ya msuli wa paja Jumapili iliyopita wakati wa mechi ambayo Chelsea walifungwa bao 1-0 na Manchester City.

Madaktari wamesema kuwa majeraha hayo mara nyingi humuweka mchezaji nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki nne mpaka nane.

Mchezaji huyo mwenye miaka 24 ambaye alisajiliwa kwa kiasi cha paundi milioni 60 akitokea Real Madrid, atakosa mechi nyingine za kombe la dunia za timu ya taifa ambapo Hispania itacheza na Albania na Israel wiki hii.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents