Michezo

Manchester City wachukua ubingwa wa Capital One

Klabu ya Manchester City jana wamechukua ubingwa Capital One baada ya kuifunga Sunderland bao 3 kwa 1.

images

Sunderland ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa na mshambuliaji wake Fabio Borini katika dakika ya kumi ya mchezo,mpaka mapumziko Sunderland ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili Manchester City ilidhamiria kupata ushindi huku wakizidisha mashambulizi langoni mwa Sunderland.

Juhudi zao zilianza kuzaa matunda, ambapo katika dakika ya 55 Yaya Toure alifyatua kombora lililotinga wavuni moja kwa moja na kuisawazishia timu yake. Dakika moja baadaye dakika ya 56, Samir Nasri alifunga bao la pili kwa mkwaju mkali na kumwaacha mlinda mlango wa Sunderland, Mannone akishangaa kinachotokea.

Jesus Navas ambaye alichukua nafasi ya Kun Aguero, alikomelea msumari wa moto katika jeneza la Sunderland baada ya kupachika goli la tatu katika dakika ya 90.Hadi mwisho wa mchezo vijana wa Pellegrini waliibuka mashujaa na kutawazwa ubingwa wa kombe hilo la Capital One, likiwa kombe lake la kwanza la ubingwa msimu huu.

Source:BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents