Michezo

Manchester City wachukua ubingwa wa Capital One

Klabu ya Manchester City wameshinda Kombe la Capital One baada ya kuwashinda Liverpool kwenye fainali kupitia mikwaju ya penalti baada ya dakika 120 kumalizika.

31A84F2800000578-3468255-image-a-94_1456687858955

Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua, Fernandinho alianza kuifungia Manchester City dakika ya 49, kabla ya Philippe Coutinho kuisawazishia Liverpool dakika ya 83.

31A85A8000000578-3468255-image-a-127_1456688704678

Shujaa alikuwa ni kipa wa Man City, Willy Caballero aliyeokoa penalti tatu na kuipa taji la Capital One kikosi cha Manuel Pellegrini, baada ya kiungo Yaya Toure kufunga penalti ya mwisho.

31A76DF300000578-3468255-image-a-71_1456684653058

31A6D04000000578-0-image-a-11_1456679373937

Emre Can pekee alifunga penalti ya Liverpool, wakati za Lucas, Philippe Coutinho na Adam Lallana zilichezwa na Caballero, huku za City zikitiwa nyavuni na Sergio Aguero, Jesus Navas na Toure, baada ya Fernandinho kukosa ya kwanza.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents