Michezo
Manchester City yakamilisha usajili wa Kevin De Bruyne
Klabu ya Manchester City ya Uingereza hatimaye imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji na klabu ya Vfl Wolfsburg ya Ujerumani, Kevin De Bruyne.
De Bruyne mwenye umri wa miaka 24, amesaini mkataba miaka sita. Amejiunga na Man City kwa ada ya pound milioni 54 na kuvunja rekodi ya usajili ya Raheem Sterling aliyechuliwa kwa ada ya pound milioni 49 kutoka Liverpool na kumleta Etihad.