Manchester City yakutana na kisiki cha mpingo EPL, Guardiola aomba ‘VAR’ Premier League
Mabingwa watetezi wa ligi kuu England klabu ya Manchester City imejikuta ikihaha kutafuta sare baada ya kupigwa bao la mapema dhidi ya Wolves mchezo uliyomalizika kwa goli 1 – 1.
Kikosi cha Man City ambacho kinaaminika kuwa miongoni mwa timu bora zaidi msimu huu imejikuta ikipata bao la kusawazisha dakika ya 69 kupitia kwa mchezaji wake, Aymeric Laporte baada ya kufungwa bao la mapema kupitia kwa Willy Boly dakika ya 57 kipindi cha pili.
Kwa matokeo hayo yanaifanya City ikipoteza alama mbili msimu huu huku Wolves ikifanikiwa kujikusanyia ponti mbili kwenye michezo yake mitatu iliyocheza.
Meneja wa Man City, Guardiola amesema kuwa licha ya kuonyesha mchezo mzuri ila anadhani kungepaswa sasa EPL kutumia mfumo wa VAR.
“Bila shaka Wolves wanastahili pongezi kuhusu goli lao siyo biashara yangu kulizungumzia hilo ila kwa namna yoyote ile Premier League inapaswa kuanza kutumia mfumo wa VAR. Wakati nazungumza na mwamuzi nilikuwa naonekana kama kama kuingilia kazi yao ,” amesema Guardiola.
Kikosi cha klabu ya Wolves: Patricio (8), Coady (6), Bennett (7), Boly (8), Doherty (6), Neves (6), Moutinho (7), Jonny (7), Jota (7), Jimenez (7), Costa (7).
Wachezaji wa akiba: Traore (7), Vinagre (NA)
Kikosi cha klabu ya Man City: Ederson (6), Walker (5), Kompany (7), Laporte (7), Mendy (6), Fernandinho (6), David Silva (6), Gundogan(7), Bernardo Silva (6), Aguero (6), Sterling (7).
Wachezaji wa akiba: Jesus (6), Sane (5), Mahrez (NA)
Mchezaji bora wa mchezo huo akiwa: Willy Boly
lig inatakiwa ivyo