Michezo

Manchester United imemtangaza nahodha wao mpya, Ole Gunnar athibitisha Rashford kuikosa Liverpool

Manchester United imemtangaza nahodha wao mpya, Ole Gunnar athibitisha Rashford kuikosa Liverpool

Kocha wa Manchester United, Ole Gunner Solskjaer amethibitisha beki Harry Maguire kuwa nahodha wa kudumu wa kikosi hicho.

Uamuzi huo wa Ole Gunnar unakuja mara baada ya aliyekuwa nahodha wa timu hiyo Ashley Young kutimukia katika klabu ya Inter Milan inayoshiriki ligi kuu nchini Italia.

Ole ameongea hayo katika mkutano na waandishi wa habari akiongelea mchezo wao wa Jumapili kati ya Manchester United dhidi ya Liverpool utakaofanyika katika dimba la Anfield linalomikiwa na Liverpool.

Mbali na hilo amethibitisha kuwa mshambuliaji wake Marcos Rashford kuukosa mchezo huo baada ya kupata majeraha katika mchezo uliochezwa katikati ya wiki kati ya Manchester United dhidi ya Wolvehampton.

Orodha ya wachezaji waliowahi kuvaa kitambaa cha Unahodha ndani ya United:
.
🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Bryan Robson
🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Steve Bruce
🇫🇷 Eric Cantona
🇮🇪 Roy Keane
🇷🇸 Nemanja Vidić
🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Wayne Rooney
🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Michael Carrick
🇪🇨 Antonio Valencia
🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Ashley Young
🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Harry Maguire 🆕

 

Chanzo SkySport.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents