Tupo Nawe

Manchester United itawagharimu kiasi hiki cha fedha endapo watamtimua, Mourinho

Klabu ya Manchester United italazimika kutoa kitita cha pauni milioni 24 kama wataamua kumfuta kazi kocha wao Jose Mourinho kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili la mwezi Januari.

Jose Mourinho is fighting to save his job at Manchester United over the busy Christmas period

Mourinho mwenye umri wa miaka 55 atalazimika kuonyesha uwezo wake wa kufundisha kwenye mchezo ujao wa ligi ya mabingwa barani Ulaya nje ya hapo watalazimika kumtimua kazi meneja huyo aliyewapatia mataji matatu makubwa.

Matokeo ya mabao 3-1 dhidi ya Liverpool wikiendi iliyopita imewafanya United kuwachwa kwa alama 19 dhidi ya vinara hao wa ligi wenye alama 45 wakiwa wamecheza jumla ya michezo 17.

Kwa mujibu wa Record Sport inaeleza kuwa United itapaswa kumlipa Mourinho mshahara wake wa mwaka mmoja wa pauni milioni 18, kama itamuwachisha kazi na kufikia hadi pauni milioni 22.5 kama timu hiyo bado itakuwa kwenye michuano ya Champions League au kwenye nafasi nne za juu.

Mourinho ameingia kwenye matatizo kabla hata kuanza kwa msimu  lakini akafanikiwa kuendelea kuwepo ndani ya klabu hiyo.

Hata hivyo baadhi ya makocha kama Zinedine Zidane na Mauricio Pochettino ni miongoni mwa wanao taja kurithi mikoba yake endapo atatimuliwa.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW