MichezoUncategorized

Manchester United na Ajax watinga fainali Europa

Manchester United wameshashinda kombe la Champions League, klabu bingwa dunia, FA na makombe mengine lakini hawajawahi kishinda kombe la Europa.

Fellaini akishangilia goli lake

United wamepata nafasi ya kutinga fainali kwa mara ya kwanza baada ya jana kutoka suluhu ya bao moja kwa moja dhidi ya Celta Vigo ya nchini Hispania.

Fainali hiyo itafanyika tarehe 24 mwezi huu katika uwanja wa Friends Arena.

Katika mchezo huo timu zote zilimaliza pungufu uwanjani baada ya Eric Bailly kwa upande wa United na Rocanglia wa Celta Vigo kuoneshwa kadi nyekundu ikiwa imebaki dakika moja kwa mchezo kumalizika.

https://youtu.be/Xz0_l5fkzwg

United walianza kupata bao dakika ya 17 baada ya Fellaini kuunganisha kwa kichwa mpira wa Marcus Rashford na bao hilo kuifanya United kwa mara ya kwanza kufunga mabao 100 katika msimu mmoja tangu mwaka 2012/2013.

Dakika zikiwa zimebaki 5 kufikia dakika ya 90 Celta Vigo walisawazisha bao hilo kupitia kwa Sebastian Rocanglia  ambaye dakika 4 baadae alipewa kadi nyekundu.

Suluhu imewafanya United kifuzu kucheza fainali kwa jumla ya mabao 2 kwa 1 kutokana na ushindi wao wa kwanza walioupata ugenini wiki iliyopita.

Fainali hii ni ya 14 kwa kocha wa United Jose katika mashindano yote toka aanze ukocha lakini rekodi yake ikiwa nzuri kwani katika fainali 13 alizowahi kufika, ameshindwa fainali 2 tu kubeba ubingwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents