Michezo

Manchester United U21 watwaa ubingwa wa ligi baada ya kuifunga Spurs

Timu ya Manchester United U21 imenyakua ubingwa wa ligi ya Uingereza kwa vijana baada ya kuifunga Tottenham kwa magoli 3-2.

manchester-united-under-21s-premier-league_3452136

Ushindi huo wa United umewafanya wachukuwe ubingwa huku wakiwa juu ya timu ya Sunderland kwa pointi mbili. United bado wana michezo miwili mkononi hawajaicheza.

Magoli ya Manchester United yalifungwa na Love dakika ya 6, Perreire dakika ya 16 na Varela dakika ya 90 huku magoli ya Spurs yalifungwa na Miller dakika ya 26 na Pritchard dakika ya 84.

GettyImages-522444932

Kikosi cha Manchester United U21 kilijumuisha wachezaji kadhaa ambao wamewahi kuichezea timu ya wakubwa, Cameron Borthwick-Jackson, Paddy McNair, Donald Love, Andreas Pereira na Varela.

Huku kwenye ligi ya wakubwa timu ya Leicester City wakiwa wanaongoza ligi na wakiwa wana matumaini ya kuchukua ligi ya Uingereza tayari timu yao ya vijana inashika nafasi ya mwisho ikiwa na pointi 18 lakini bado haijacheza mechi mbili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents