Habari

Manchester United VS Chelsea: Je! Utata utaisha?

Baada ya mechi ya English Premier League kati ya Chelsea na Manchester United kuisha kwa utata wa namna ambavyo asilimia kubwa ilionekana refa wa mchezo huo Mark Clattenburg kuwabeba Man United na hivyo kuchangia ushindi wa timu hiyo siku ya Jumapili usiku, timu hizo zinakutana tena leo usiku katika mtanange ambao wengi wanaamini utamaliza ubishi wa Je! ni kweli Man U wanabebwa na marefa wanaochezesha ligi Uingereza?

Timu hizo mbili zenye upinzani wa hali ya juu katika karne hii, zinakutana siku mbili baada ya kupambana katika mechi ya ligi kuu na mara hii zikikutana katika mpambano wa mtoano wa michuano ya chama cha soka cha Uingereza FA.

Habari ambayo imetawala vinywa vingi ni namna ambavyo wapenzi wengi wa soka hasa hasa wale mahasimu wa Man United kama Arsenal, Liverpool, Chelsea yenyewe n.k wanavyoamini kwamba kama si kwa kubebwa Man U haiwezi kuifunga Chelsea na kwakuwa ilishindwa kuwafunga Chelsea kwa miaka kumi.

Je! Manchester United itabebwa tena au Chelsea watathibitisha kwamba walionewa? Tupe maoni yako mdau wa soka la Uingereza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents