Manchester United yakamilisha usajili wa mlindalango wa Stoke

Aliyekuwa mlindalango wa klabu ya Stoke, Lee Grant amekamilisha usajili wa kutua Manchester United kwa dili la miaka miwili.

Grant mwenye umri wa miaka 35 alionekana juzi siku ya Jumatatu kwenye viunga vya Carrington kwaajili ya kufanyiwa vipimo vya afya ili kukamilisha usajili huo wa dau la pauni milioni 1.5.

Stoke ipo kwenye mazungumzo na Adam Federici kutoka Bournemouth ili kupata mbadala wake.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW