Michezo

Manchester United yamalizana na Ibrahimovic

Hatimaye timu ya Manchester United imekamilisha rasmi usajili wa aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Sweden, Zlatan Ibrahimovic.

13267349_246663199026538_1940231266_n

Mpaka sasa mchezaji huyo amefanikiwa kucheza jumla ya mechi 611 tangu ameanza kucheza soka na kufunga jumla ya magoli 371. Pia aliwahi kucheza kwenye timu kadhaa ikiwemo Ajax, Malmo, Juventus, Inter Milan, Barcelona AC Milan, PSG, timu ya taifa ya Sweden ya vijana na wakubwa.

Baada ya kusaini mkataba huo wa kuichezea United “Nina furaha kubwa kujiunga na Manchester United,” alisema Ibrahimovic. “Nasubiri kwa hamu kuanza kwa msimu mpya wa Ligi ya England na kucheza kwa mara ya kwanza.”

Aliongeza “Sitakuwa muungwana kama sitabainisha furaha yangu ya kuungana kwa mara nyingine tena Jose Mourinho. Ni kocha mzuri na nipo tayari kupata changamoto mpya kutoka kwake. Mara nyingi nimekuwa nikifurahia maisha yangu ya soka mpaka sasa na nina kumbukumbu nzuri nyingi sana. Na sasa nakuja England kuweka kumbukumbu nyingine tena .”

Naye kocha wa timu hiyo, Jose Mourinho alisema kuwa mchezaji huyo hahitaji utambulisho kwa kuwa takwimu zimeweka wazi uwezo wa Ibra kuwa ni mmoja kati ya washambuliaji bora kwa sasa ulimwenguni na amekuwa akijitolea kwenye timu yake kwa asilimia 100.

“Amefanikiwa kushinda ubingwa muhimu wa ligi katika ulimwengu wa soka, na sasa ana fursa nyingine ya kucheza katika ligi bora kabisa ulimwenguni na naamini atatumia fursa hii kufanya kila awezalo kuisaidia timu kushinda mataji. Naamini kwamba kipaji chake kitawapa furaha kubwa mashabiki wa United katika dimba la Old Trafford msimu ujao na uzoefu wake pia utakuwa na thamami kubwa katika kutoa mchango kwa wachezaji vijana katika timu,” alisema Mourinho.

Ibrahimovic ni mchezaji wa pili kusajiliwa na Jose Mourinho tangu alipotangazwa kuwa kocha mkuu wa timu hiyo huku usajili wake wa kwanza ulikuwa kwa beki wa Villarreal, Eric Bailly.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents